Airtel yawazawadia washindi wa TESA KIMILIONEA ZAIDI gari mpya Toyota Rav4 pamoja na Tshs 10 milioni

.-TESA KIMILIONEA ilikuwa ni wateja na mawakala wa Airtel Money kote nchini.

Dar es Salaam, Jumanne 20 Julai 2022: Airtel Tanzania leo imekabididhi zawadi kwa washindi wawili wa droo kubwa ya promosheni ya TESA KIMILIONEA INAEDELEA, mshindi mmoja amekabidhiwa gari mpya aina ya Toyota RAV4 na wa pili pesa taslimu Tshs 10 milioni.

Washindi hao ni John Mathayo, mkazi wa Bunju na mfanya biashara wa nyanya na Ibrahim Dyamwala ambaye ni mkazi wa Goba jijini Dar es Salaam.

Wateja na Mawakala walikuwa na nafasi ya kuingia kwenye droo ya kwa kutumia moja ya huduma za kuweka pesa, kutuma pesa Airtel kwenda Airtel, kutoa pesa, kulipia bili kwa kutumia huduma ya Airtel Money ya promosheni ya TESA ZAIDI KIMILIONEA na kujishindia Tshs 1 milioni kila siku au gari mpya aina ya Toyota RAV4 na pesa taslimu Tshs 10 milioni kwenye droo kubwa.

Kwa upande wake, mshindi wa zawadi ya Tshs 10 milioni Ibrahim Dyamwala alisema ‘Nilikuwa siamini kama ni kweli Naweza kuwa nimeshinda hii zawadi ya Tshs 10 milioni. Kwa leo nimeamini na nawashukuru Airtel kwani kwa sasa nitaweza kukamilisha ujenzi wa nyumba yangu pamoja na kuongeza uwekezaji kwenye kilimo. Naomba kuwahidi kuwa nitaendelea kutumia bidhaa za Airtel pamoja na kuwahimiza ndugu, jamaa na marafiki juu ya umuhimu wa kutumia Airtel Money.

Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda (kulia) akimkabidhi mfano wa ufunguo wa gari aina ya Toyota RAV4 mshindi wa droo kubwa ya TESA KIMILIONEA INAENDELEA John Mathayo ambaye ni mkazi wa Bunju jijini Dar es Salaam. Promosheni ya TESA KIMILIONEA INAENDELEA ilikuwa inawapa fursa wateja na mawakala wa Airtel Money ya kujishindia Tshs 1 milioni kila siku au gari mpya aina ya Toyota RAV4 pamoja na pesa taslimu Tshs 10 milioni kwenye droo kubwa ya mwisho kila wana wanavyofanya muamala wowote kwa kutumia huduma ya Airtel Money


Mkurugenzi wa Huduma za Airtel Money Isack Nchunda (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Tshs 10 milioni Ibrahim Dyamwala ambaye ni mshindi wa droo kubwa ya TESA KIMILIONEA INAENDELEA leo jijini Dar es Salaam. Promosheni ya TESA KIMILIONEA INAENDELEA ilikuwa inawapa fursa wateja na mawakala wa Airtel Money ya kujishindia Tshs 1 milioni kila siku au gari mpya aina ya Toyota RAV4 pamoja na pesa taslimu Tshs 10 milioni kwenye droo kubwa ya mwisho kila wana wanavyofanya muamala wowote kwa kutumia huduma ya Airtel Money. Kulia ni Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando na wa pili kushoto ni Meneja Huduma za Airtel Money Maria Mwamyalla.

No comments: