MGANA NA WATANZANIA WATATU KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI

 



RAIA mmoja wa Ghana na watanzania watatu wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ua uhujumu uchumi yenye mashtaka manne likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya Sh. Bilioni mbili.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Tumaini Mafuru imewataja washtakiwa hao kuwa ni Valentine Kof (45) raia wa Ghana anayeishi Mikocheni, Patrick Tarimo(34) mkazi wa Kibaha, Aisha Kagashe (40) anayeishi SInza na Idan Msuya (46), mkazi wa Mikocheni.

Washtakiwa hao ambao wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Jofrey Mhini, katika shtaka la kwanza wanadaiwa kutenda kosa la kuongoza genge la uhalifu kati ya Septemba Mosi 2021 na Oktoba

25, 2021 huko katika maeneo ya Arusha na Dar Es Salaam nchini Tanzania, Ghana, Ivory Coast, Uganda, Zambia, Senegal, Cameroon, France Mali na Burkina Faso

Inadaiwa katika kipindi hicho washtakiwa wakiwa pamoja na watu wengine ambao hawapo mahakamani waliongoza genge la uhalifu kwa kuingilia mfumo wa kompyuta wa benki ya African Banking Corporation Tanzania Ltd (Bank ABC) kinyume cha sheria kwa lengo la kutenda kosa la wizi na hivyo waliiba Sh. 2,095,170,000

katika shtaka la pili imedaiwa katika kipindi hicho hicho washtakiwa kwa pamoja wakiwa na watu wengine ambao hawapo mahakamani kwa makusudi walisababisha mfumo wa ABC benki kuingiliwa na Akaunti ya Visa ya malipo ya awali (Pre-Paid Visa) ipokee malipo ya Sh. 3,543,555,243'37

Wakili Mafuru ameendelea kudai kuwa katika tarehe hizo na mhali hapo hapo washtakiwa waliiba Sh. 2,095,170,000 kwa njia ya kuzitoa kupitia mfumo wa Kadi ya Visa ya malipo ya awali (Pre-Paid Visa) kutoka kwenye utambulisho wa benki namba (BIN) 486054 mali Benki hiyo

Washtakiwa pia wanakabiliwa na shtka la utakatishaji ambapo wanadaiwa kujipatia kiasi che fedha hizo zaidi ya Sh. Bilioni mbili mali ya benki hiyo wakati wakijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la wizi.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na washtakiwa wamerudishwa rumande hadi Machi 26,2025 kesi hiyo Itakapokuja kwa ajili ya kutajwa

Leave a Comment

No comments: