Wasomi wasema uchumi wa ‘Blue’kuipaisha Zanzibar
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
AZMA ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Hussein Ali Mwinyi ya kujenga uchumi wa ‘Blue’ umewaibua wasomi na wataalamu mbalimbali hapa nchini wakipongeza na kusema mafanikio ya utekelezaji wake yataupaisha uchumi na maendeleo ya visiwa hivyo kwa haraka.
Tangu alipoingia madarakani mwaka 2020, Rais Mwinyi aliweka bayana azma ya serikali yake kutumia fursa lukuki zinavizunguka visiwa hivyo zikiwemo fukwe, uvuvi, kilimo cha mwani sambamba na mazao ya baharini.
“Zanzibar imebarikiwa kuwa na fukwe nyingi ambazo ni nzuri kwa uwekezaji wa mahoteli na vivutio mbalimbali kwa utalii. Kinachotakiwa hapa uungaji mkono wa wazanzibari wote katika kufanikisha hilo,” Sadiki Mbarouk Mahamudi,” alisema na kutaka wananchi wahamasishwe Zaidi kuona fursa hizo.
Bw Mahamudi ambaye ni mbobezi katika masuala ya uchumi na uwekezaji alisema fursa zinazoizunguka Zanzibar ni nyingi sana kuliko Zanzibar yenyewe na hivyo kuipongeza serikali kwa kuliona hilo katika awamu hii ya uongozi.
Dkt Tasco Luambano ambaye ni Mhadhiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya alisema uamuzi wa Rais Mwinyi kuunda Wizara Maalumu inayoshughulikia masuala ya Uchumi wa ‘Blue’ inatoa tafsiri ya halisi ya maono ya kiongozi huyo katika kuiletea Zanzibar mageuzi stahiki ya kiuchumi.
“Hatua ambazo Rais Mwinyi amezichukua tangu aangie madarakani zimelenga kuibadilisha na kuipaisha Zanzibar kiuchumi na kimaendeleo. Mwenye macho hapaswi kuambiwa aone kwani Zanzibar ya 2020 siyo ya 2022,” alisema.
Dkt Luambano ambaye huenda Zanzibar mara kwa mara alipongeza juhudi anazochukua Rais Mwinyi kuhakikisha kuwa mazao na raslimali zinazotokana na bahari zinatumika kuijenga Zanzibar na kuwaletea wananchi maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Dkt. Zubeda Salim Abdallah alisema uchumi wa ‘Blue’ ni njia sahihi ya kujenga uchumi imara kwa Zanzibar kwani kupitia mazao ya bahari, uvuvi na raslimali zote zinazovizunguka visiwa hivyo maisha ya wazanzibari wote yatabadilka kwa haraka.
“Uchumi wa ‘Blue’ ni msingi wa kujenga sekta zingine za uchumi zikiwemo sekta za utalii na huduma, viwanda, miundombino, mawasiliano ,elimu, afya na nyinginezo nyingi,” alisema Dkt Zubeda ni mhadhari wa uchumi na mwenyeji wa Pemba.
Walimtaka Rais Mwinyi kusimamia maumuzi yake kama alivyofanya Rais mstaafu wa Zanzibar Dkt Salmin Amour alipoamua ujenzi wa mahoteli alipingwa sana na baadhi ya watu bila kujua matokeo ya baadaye na kwasasa matunda ya uwekezaji huo yanaonekana ambapo serikali inakusanya mapato mengi kupitia tasnia hiyo.
Hivi karibuni, viongozi wastaafu walikemea habari za upotoshaji kuwa Rais ameuza visiwa kama sehemu ya kumkatisha tamaa na juhudi za serikali yake kuhamasisha uwekezaji kwenye fukwe ilikuchochea ukuaji wa uchumi.
Hatahivyo, wastaafu hao walikwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa Zanzibar haina madini na kutegemea zaidi uchumi unaotokana mazao ya bahari na kilimo na kumtaka Rais Mwinyi kuendelea kuvutia uwekezaji kwenye fukwe ambao utasaidia kuongeza vipato kwa wakazi wa maeneo husika.
Kauli hizo za viongozi ndani ya chama vimekuja kufuatia baadhi ya viongozi wastaafu ndani ya chama kuleta migongano na mivutano isiyo ya lazima na kushindwa kuwaunga mkono viongozi waliopo waweze kutekeleza majumu yao.
No comments: