RUANGWA JIMBO CUP YAIBUA 7 KWENDA NAMUNGO-20



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa akimkabidhi kikombe cha ubingwa wa mpira wa miguu katika jimbo hilo, Nahodha wa Mkeng’ende FC, Hassan Mineng’ene baada ya timu hiyo kuibugiza Mkangano FC 5-1 katika mechi ya fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids, Ruangwa, Septemba 4, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Ally Lipapa wa Mkeng’ende FC (kulia) akichuana na Saidi Ahmed wa Mkangano FC katika mechi ya fainali ya kuwania kombe la Jimbo la Ruangwa iliyochezwa kwenye uwanja wa Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kinds, Ruangwa Septemba 4, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa kombe la Jimbo la Ruangwa la Jimbo la Ruangwa, Mkeng’ende FC katika mechi ya fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids, Ruangwa, Septemba 4, 2021. Katika mechi hiyo Mkeng’ende waliwafunga Mkangano FC, 5-1. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Mabingwa wa mpira wa miguu wa kombe la Jimbo la Ruangwa Mkeng’ende FC wakifurahia ushindi baada ya kukabidhiwa kikombe cha ubingwa wa Jimbo la Ruangwa baada ya kuifunga Mkangano FC 5-1. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Kipa wa Mkeng’ende FC, Athumani Kasambila akipangua mpira wa kona katika mechi ya fainali za kombe la Jimbo la Ruangwa ambapo timu hiyo iliifunga Mkangano FC 5-1. Kushoto ni Athumani Nuochochola wa Mkangano. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

*****************************************

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa ameshuhudia mechi ya fainali ya mashindano kuwania kombe la Jimbo la Ruangwa ambapo Nkeng’ende FC iliichapa Mkangano FC 5-1.

Katika mechi hiyo iliyochezwa jana (Septemba 4, 20201) kwenye uwanja Shule ya Awali Msingi ya Wonder Kids, Mheshimiwa Majaliwa alisoma majina saba ya wachezaji ambao watajiunga na kambi ya timu ya vijana ya chini ya miaka 20 ya Namungo FC.

Waziri Mkuu alisema kuwa lengo la masindano hayo lilikuwa ni kuuibua vipaji kwa vijana ambao baadae wataichezea Namungo FC ya wilani Ruangwa.

Mashindano ya kuwania kombe la Jimbo la Ruangwa yalishirikisha 32 kutoka Kata za Jimbo hilo ambapo mshindi wa kwanza alipata kombe, kitita cha sh. milioni mbili, seti moja ya jezi na mpira.

Mshindi wa pili alijipatia shilingi Milioni Moja na nusu, seti moja ya jezi na mpira na mshindi wa tatu shilingi milioni moja, seti moja ya jezi na mpira.

Wakizungumza baada ya kuwa wametajwa kuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji wa Namungo chini ya miaka 20, vijana hao wamepongeza maandalizi ya michuano hiyo nakuahidi kutumia fursa waliyoipata katika kuinua kiwango cha soka kwenye timu hiyo na Jimbo la Ruangwa.

Naye, Kapteni wa Timu ya Nkeng’ende FC alisema siri ya wao kuchukua ubingwa ni maandalizi waliyoyafanya katika kipindi chote cha michuano pamoja na nguvu ya mashabiki ambao walijitokeza muda wote wa michuano

No comments: