JUMUIYA YA ZAFELA KUFANYA UZINDUZI MAALUM UTAKAOLENGA KUIHAMASISHA JAMII KUWAUNGA MKONO WANAWAKE

 Mkurugenzi wa Jumuia ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) Jamila Mahmoud Juma amesema Jumuia hio kupitia mradi wa ushirikishwahaji wanawake katika uongozi (SWIL) wanategemea kufanya uzinduzi wa mkutano maalumu utakaolenga kuihamasisha jamii kuwaunga mkono wanawake kushika nafasi za uongozi katika viwanja vya kisonge Jumapili ya septemba 5 mwaka huu.

 Ameyasema hayo alipokua akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho zilizopo Mpendae mjini Unguja wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali mjini hapa.

 Alisema katika mkutano huo mgeni rasmi wanatarajiwa kuwa Waziri wa TAMISEMI Massoud Ali Mohamed, huku lengo kuu la mkutano huo ni kuihamasisha jamii kufahamu kuwa wanawake ni watu wanaostahiki kuwa viongozi kama walivyo wanaume.

 Alisema baada ya kuzinduliwa kwa mkutano huo mikutano mengine itafanyika katika mikoa yote ya Unguja na kuwataka wananchi kujitokeza pale watakapopata taarifa za mikutano hio,ambapo kwa mkoa wa kaskazini mkutano huo unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 11 mwezi huu na kusini  tarehe 18.

 Alisema kutokana  na changamoto  nyingi visiwani hapa ambazo  zinawakabili wanawake wengi wenye dhamira ya kupata nafasi za uongozi, wanaamini kuwa kupitia mpango huo jamii itahamasika na kuwaunga mkono wanawake wengi hatimae wanawake walio wengi kushika nafasi ziwe za kisiasa au hata za kijamii.

 Alieleza kuwa visiwani Zanzibar ushiriki wa wanawake katika nafasi za maamuzi hasa ya kisiasa bado ni mdogo hali ambayo inakinzana na azma ya kujenga jamii isokuwa na ubaguzi  kama ilivyobainishwa kwenye dira ya Taifa  2017-2022,katiba ya Zanzibar yam waka 1984 pamoja na sheria mbali mbali za Nchi zinazosisitiza usawa wa kijinsia.

 Katika hatua nyengine Mkurugenzi huyo alisema tayari wameshawajengea uwezo vijana 60 kutoka maeneo mbali mbali ambao watafanya kazi ya kuhamasisa jamii katika kuwaunga mkono wanawake waweze kushika nafasi za uongozi.

 Awali mratib wa mradi huo kutoka TAMWA-ZNZ Salma Amir Lusangi alisema mradi huo unalenga kuwafikia wanawake elfu sita kutika wilaya zote za Unguja na Pemba.

 Alisema mradi huo  wa miaka mine unatekelezwa na TAMWA-ZNZ kwa  kwa kushirikiana na PEGAO pamoja na ZAFELA chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Norway Nchini Tanzania.

Mkurugenzi wa Jumua ya Wanasheria wanawake Zanzibar (ZAFELA) Jamila Mahmoud (katikati)kushoto mratib wa mradi wa kuwawezesa wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi Khairat Hamid na kulia ni mratib wa mradi huo kutoka TAMWA-ZNZ Salma Amir Lusangi walipokua wakizungumza na waandishi wa habari.


 .Mratib wa mradi huo kutoka ZAFELA Khairat Hamid akitoa akifungua mkutano wa waandishi wa habari,katikati ni Mkurugenzi wa ZAFELA Jamila Mahmoud na mwengine ni mratib wa mradi huo kutoka TAMWA-ZNZ Salma Amir Lusangi.



No comments: