UJUMBE WA TANZANIA NCHINI CAPE VERDE KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA WA UTALII
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akimuonesha baadhi ya vivutio vya utalii vilivyopo katika jarida la Utalii kutoka Tanzania Waziri wa Utalii wa Hispania, Maria Illerakabla ya kumkabidhi zawadi ya majarida yanayoelezea utajiri wa vivutio vya utalii vilivyopo nchini mara baada kufanya kikao cha ana kwa ana kando ya mkutano wa 64 Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika unaoendelea kufanyika kwa muda wa siku nne katika Kisiwa cha SAL nchini Cape Verde
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akimkabidhi zawadi ya Kijitabu cha misitu kinachoelezea fursa za uwekezaji katika maeneo ya misitu nchini Mhe. Ngobitizitha Ndlovu (kushoto) mara baada kufanya kikao cha ana kwa ana kando ya mkutano huo wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika unaoendelea kufanyika kwa muda wa siku nne katika Kisiwa cha SAL nchini Cape Verde
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ( katikati ) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Utalii na Mambo Kale Zanzibar, Mhe.Lela Mussa Mohamed (kushoto) pamoja na Waziri wa Utalii wa Morroco Mhe.Nadia Fettah ( kulia) mara baada kufanya kikao cha ana kwa ana kando ya mkutano huo wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika unaoendelea kufanyika kwa muda wa siku nne katika Kisiwa cha SAL nchini Cape Verde
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiagana na Waziri wa Utali Cape Verde, Mhe. Carlos Santos akiagana na Waziri wa Utalii wa Cape Verde….. ambapo wamekubaliana katika kubadilishana uzoefu katika kukuza utalii
No comments: