REMTULAH AWAPONGEZA WADAU WANAOTHAMINI KAZI ZA WABUNIFU

 Na.khadija Seif, Michuzi Tv

MKONGWE kwenye tasnia ya ubunifu ameiomba Serikali kupunguza bei za  Malighafi kwa ajili ya kutengeneza nguo ili kuendelea kuvipenda vya nyumbani zaidi.

Akizungumza na Michuzi Tv, Mbunifu wa Mavazi kwa miaka takribani 15 Ally Remtullah amesema anawapongeza Sana wadau mbalimbali wanaoendelea kutoa ushirikiano na kununua kazi za wabunifu hao hususani viongozi,wasanii pamoja na Wana Michezo huku akitoa wito kwa Serikali kupunguza Bei za Malighafi ili iwe rahisi hata baadhi ya nguo kutengenezwa hapa nyumbani.

"Sheria ngowi amebuni jezi ya timu ya Yanga ni kitu kizuri kwa namna moja au nyingine inaonyesha wazi kuwa wabunifu tunaendelea kupewa nafasi katika jamii lakini ingependeza zaidi jezi hiyo ingetengenezwa hapa hapa nchini ila kutokana na kuwepo kwa shida ya baadhi ya Malighafi imelazimika jezi hiyo kutengenezwa nje ya nchi."

Pia amesema kwa Sasa amejikita zaidi kusaidia wabunifu chipukizi kwa kupitia darasa lake alilolipa jina la "Remtulah 010 " ikijumuisha wabunifu wakubwa pamoja na watoto.

"Ni darasa ambalo linafanyika kwa miezi mitatu yenye vitendo na Nina wapa nafasi kuwaandalia jukwaa la kuonyesha kazi ama vitu ambavyo wamebunia kuanzia watoto pamoja na wakubwa na katika darasa Hilo watoto ni bure kabisa hakuna malipo."

Hata hivyo amesema kupitia darasa Hilo linampa nafasi mkufunzi kujitangaza kibiashara.



No comments: