BARRICK YATOA MSAADA WA PIKIPIKI KUWEZESHA UKAGUZI WA MIRADI YA KIJAMII WILAYANI NYANG’WALE,GEITA.
Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita , Bw. David William Jamhuri (Kushoto) akipokea msaada wa pikipiki 8 kutoka kwa mrakibu idara ya mahusiano wa Barrick Bulynhulu, William Chungu, zilizotolewa na kampuni kwa ajili ya kuwezesha maofisa wa Serikali wilayani humo kutembelea miradi ya kijamii.
Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, Bw. David William Jamhuri (Kulia) akipokea msaada wa pikipiki 8 kutoka kwa mrakibu idara ya mahusiano wa Barrick Bulynhulu, William Chungu, zilizotolewa na kampuni kwa ajili ya kuwezesha maofisa wa Serikali wilayani humo kutembelea miradi ya kijamii
Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, Bw. David William Jamhuri (kulia) na Mkurugenzi wa Manispaa ya hiyo Husna Tonny Chambo, wakiangalia pikipiki 8 zilizotolewa na kampuni ya Barrick mgodi wa Bulyanhulu
Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita , Bw. David William Jamhuri akijaribu kuendesha moja ya pikipiki zilizotolewa na Barrick.
***
Kampuni ya Barrick imetoa msaada wa pikipiki 8 kwa ajili ya kufanikisha ukaguzi wa miradi ya kijamii wilayani Nyang’hwale iliyopo mkoani Geita.
Barrick kupitia sera yake ya kusaidia huduma za jamii katika maeneo yanayozunguka maeneo yake ya kazi (CSR), inafadhili miradi mbalimbali ya kijamii wilayani humo.
Msaada huo ulikabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya hiyo ,David Jamhuri .ilihudhuriwa na wafanyakazi wa Serikali wilayani humo na wafanyakazi waliowakilisha kampuni ya Barrick.
No comments: