MATUKIO KATIKA PICHA ZOEZI LA UHAKIKI WA VYAMA VYA SIASA LIKIENDELEA

 

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Ndg. Sisty Nyahoza akimuelekeza jambo Mweka Hazina wa Chama Cha Kijamii (CCK), Bibi. Mariam Mnkande walipotembelea Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo Mtaa wa Kapera, Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam kwa ajili ya zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa mapema hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Kijamii (CCK), Ndg. Joachim Hugo Mwakitiga akielezea jambo mbele ya wajumbe wa Kikosi Kazi cha Zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Siasa walipotembelea Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo Mtaa wa Kapera, Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam kwa ajili ya zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa mapema hivi karibuni. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama hicho, Ndg.David Daud  Mwaijojele na kulia ni Mweka Hazina Bibi. Mariam Mnkande.

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Ndg. Sisty Nyahoza (wa pili kushoto waliokaa) pamoja na wawakilishi wa Ofisi ya Msajili wengine wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama Cha Kijamii (CCK) mara baada ya kukamilisha zoezi la uhakiki wa uhai wa chama hicho mapema hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini, Ndg. Amir Hassan Amir akiwaonyesha wajumbe wa kikosi kazi cha zoezi la uhakiki wa Vyma vya Siasa toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa walipotembelea Ofisi za Chama hicho kwa ajili ya zoezi hilo mapema hivi Karibuni.

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Ndg. Sisty Nyahoza(kushoto) akikagua rejesta ya wanachama wa Chama cha Demokrasia Makini wakati wa zoezi la Uhakiki wa Vyama vya Siasa mapema hivi karibuni. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama hichi Ndg. Amir Hassan Amir.

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Ndg. Sisty Nyahoza(aliyevaa barakoa) akitoa neon la pongezi kwa uongozi wa Chama cha Demokrasia Mkini kwa kutekeleza maelekezo ya kutumia mfumo wa TEHAMA katika kurejista wanachama. Kulia ni Katibu  Mkuu wa Chama hicho Ndg. Amir Hassan Amir na Katibu Mwenezi Taifa, Ndg. Salum J. Elias.

Pichani ni muonekano wa Rejesta ya wanachama wa Chama cha Demokrasia Makini kwa kutumia mfumo wa TEHAMA.

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Ndg. Sisty Nyahoza (wa pili kushoto waliokaa) pamoja na wawakilishi wa Ofisi ya Msajili wengine wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Demokrasia Makini mara baada ya kukamilisha zoezi la uhakiki wa katika chama hicho mapema hivi karibuni. (Picha na: ORPP)

No comments: