KOKA AIPIGA JEKI YA MADAWATI 2O SHULE YA MSINGI MUUNGANO ILIYOCHOMWA MOTO KIBAHA Inbox
NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Mbunge wa Kibaha Mjini Mhe Silyvestry Koka jana amefanya ziara ya kutembelea shule ya msingi Muungano iliyopo kata ya Kibaha iliyochomwa moto na watu wasiojulikana hivi karibuni na kuahidi kuchangia madawti 20.
Afisa mtendaji wa mtaa wa kwamfipa Kuboja Majogoro amemweleza Mbunge kuwa kwa kushirikiana na wananchi walifanya jitihada kadhaa za kuinusuru ikiwa ni pamoja na kuwaita jeshi la zimamoto lakn tayari jengo la madarasa mawili na ofisi yalikuwa yameshaungua.
Koka baada ya kukagua uharibifu ambao umejitokeza amewahakikishia wananchi kuwa tayari Halmshauri ya mji kibaha imeshaingiza kiasi Cha shilingi 19,200,000/- kwenye akaunti ya shule kwa ajili ya ukarabati ambao tumeshaanza.
Pia Koka alisema kwamba nia ya serikali ni kuhakikisha inabooresha sekta ya elimu kwa kuwajengea mazingira rafiki wanafunzi ili waweze kufanya vizuri na kwamba hawezi kulifumbia macho suala la vitendo vya uharifu unaofanyika hasa kwa kuchoma Moto shule na nyumba za watu.
Wakati huo huo Mbunge ametembelea wahanga wa ajali ya moto kata ya kongowe iliyopelekea familia moja kumpoteza kijana wa miaka 22. Akitoa salamu za rambirambi amewaomba wafiwa kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu Cha majonzi.
Kufuatia matukio hayo ya moto Koka akiwa ziarani humo alimpigia simu OCD Kibaha kujua kuna mkakati gani wa kuimarisha ulinzi pamoja na kuwaelimisha wananchi kuwa na ulinzi shirikishi.
Pia Mbunge Koka amesema amechukizwa na Jambo Hilo la baadhi ya waharifu kuchoma Moto shule hiyo ya msingi na kuwataja wanachi wa kibaha kutolifumbia macho hata kidogo na kwamba watoe taarifa na kuwafichua wale wote ambao wanajihusisha na vitendo hivyo.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka wa Kati Kati akiwa na baadhi ya viongozi wa Chama chama mapinduzi CCM wakati alipowatembelea wahanga waliounguliwa na nyumba yao kata ya kongowe.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka wa kulia wakati alipokwenda kutembelea shule ya msingi Muungano ambayo ilichomwa Moto na watu wasiojulikana.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
No comments: