DAWASA YAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA KWA KUPANDA MITI 1000 RUVU CHINI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeungana na wadau wa Mazingira kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani kwa kupanda miti elfu moja kando kando ya chanzo cha Maji Ruvu chini wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Zoezi la upandaji mita limefanywa na watumishi wa Mamlaka likiwa na lengo la kuendelea kuboresha Mazingira yaliyoharibiwa kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu zinazofanywa katika vyanzo na kingo za mto.
Akizungumza katika zoezi hilo, Mkuu wa idara ya Mazingira Mhandisi Modesta Mushi amesema Sambamba na zoezi hilo la kupanda miti DAWASA inaendelea kutoa elimu kwa wakazi wa maeneo hayo na kuwashauri jinsi ya kutafuta shughuli mbadala kama vile ufugaji nyuki kwa ajili ya uzalishaji wa asali ili kuacha kufanya shughuli za kilimo katika vyanzo vya Maji.
"Utunzaji wa Mazingira katika vyanzo vya maji ni kipaumbele cha Mamlaka ili kuhakikisha kwamba vyanzo vya maji havikauki hali ambayo ikitokea hupelekea kuwepo kwa upungufu wa uzalishaji wa maji." alisema Mhandisi Modesta
Siku ya Mazingira huadhimishwa kila tarehe 5 ya mwezi Juni na mwaka huu kauli mbiu ni "tutumie nishati mbadala kuongoa mfumo ekolojia"
Afisa Mazingira kutoka DAWASA, Valence Lyamuya akitoa ufafanuzi wakati wa kuanza kwa zoezi la upandaji wa miti kando kando ya chanzo cha Maji Ruvu Chini wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani.
Mkuu wa kitengo cha Mazingira DAWASA, Mhandisi Modester Mushi akipanda mti kando kando ya chanzo cha Maji Ruvu Chini wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani.
Meneja Mawasiliano DAWASA, Everlasting Lyaro akipanda mti kando kando ya chanzo cha Maji Ruvu Chini wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani.
Baadhi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) pamoja na wadau wa Mazingira wakipanda miti kando kando ya chanzo cha Maji Ruvu Chini wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani.
Mkuu wa kitengo cha Mazingira Mhandisi Modester Mushi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kupanda miti katika vyanzo vya maji ili kuokoa upotevu wa maji wakati wa siku ya Mazingira Duniani kwa kupanda miti elfu moja kando kando ya chanzo cha Maji Ruvu chini wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini DAWASA Mhandisi Emaculata Paul akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna wanavyokabiliana na changamoto za utunzaji wa mazingira katika eneo la mto huo kwa ajili ya upatikanaji wa maji mengi yatakayoweza kutumiwa na wananchi wa Dar es Salaam pamoja na Bagamoyo wakati wa siku ya maadhimisho ya wiki ya maji inayohadhimishwa tarehe 05 kila mwaka.
Meneja Mawasiliano DAWASA, Everlasting Lyaro akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna DAWASA walivyoadhimisha siku ya Mazingira Duniani kwa kupanda miti elfu moja kando kando ya chanzo cha Maji Ruvu chini wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani
Baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na kituo cha uzalishaji wa maji cha Ruvu Chini wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upandaji miti katika eneo la mto ili kuweza kulinda mazingira ya mto huo.
No comments: