WAJASIRIAMALI WENYE VIWANDA JIJINI ARUSHA WALIA NA GHARAMA KUBWA ZA USAJILI

Na Woinde Shizza , Michuzi Tv-ARUSHA

WAJASIRIAMALI wenye viwanda Mkoani hapa,wamelalamikia gharama kubwa za usajili  wanazotozwa na taasisi za serikali pindi wanapotaka kuanzisha viwanda vipya hali ambayo imekuwa ni kikwazo kikubwa kwao

Wameeleza kuwa gharama hizo ni zile wanazotakiwa kulipa pindi wafuatiliapo vibali vya kuanzisha viwanda,leseni pamoja na ukiritimba wanaohupata katika shirika la viwangi nchini(TBS)pamoja na mamlaka ya dawa na vifaa tiba(TMDA)wanapohotaji kusajili bidhaa zao

Waliyasema hayo leo walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari katika mafunzo ya Kaizen,yana yoendelea katika ofisi za shirika la kuhudumia viwanda vidogo nchini(SIDO),Mkoani hapa.

Mafunzo hayo yaliyowakutanisha wamiliki na wasimamizi wa viwanda vidogo 70,kutoka Mkoani hapa yalifadhiliwa na Mfuko wa kuendeleza ujuzi (SDF) ulioko chini ya mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na kuendeshwa na SIDO.

Mmiliki wa kiwanda cha kuchakata vyakula vya mifugo cha Mushono Farms,Hulda Kombe alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikiwakatisha tamaa na kuwapa wakati mgumu katika kuendana na juhudi za serikali za Tanzania ya Viwanda.

“Kwanza tunampongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ,Dkt,John Magufuli kwa kutambua mchango wa wajasirimali na kutaka Tanzania iwe ya viwanda, ila baadhi ya Taasisi za serikali zimekuwa zikimkwamisha hivyo tunamuomba aliangalie jambo hili”alisema.

Kombe aliongeza kuwa changamoto nyingine ambazo wamekuwa wakikumbana nazo katika juhudi zao za kuanzisha viwanda ni riba kubwa wanazotozwa na taasisi za kifedha pindi waombapo mkopo kwa ajili ya kukuza mitaji yao na kuiomba serikali kuwapatia mikopo isiyo na riba.

Alilipongeza shirika la kuhudumia viwanda vidogo(SIDO),Mkoani hapa kwa mafunzi hayo na kueleza kuwa wamejifunza kuzalisha bidhaa bora zenye tija na viwango kwa mida mfupi na kwa gharama nafuu ikilinganishwa na hapo awali.

“Pia SIDO wametufundisha namna ya kutatua changamoto mbalimbali tunazokutana nazo viwandani na sokoni na baada ya mafunzo haya uzalishaji wenye tija na viwango utaongezeka katika viwanda vyetu”alisema Mmiliki huyo wa moshono Farms.

Naye Richard Njuga kutoka kiwanda cha uzalishaji wa dawa za mifugo alisema kuwa changamoto kubwa anayokumbana nayo yeye ni gharama kubwa za malighafi,mitaji ambapo pia ameiomba serikali ipunguze gharama za usajili wa bidhaa.


 

No comments: