TANZANIA NA HUNGARY ZAINGIA MAKUBALIANO UFADHILI WA MASOMO KWA WANAFUNZI

 






DESEMBA 7 mwaka huu, Serikali za Tanzania na Hungary zilitiliana Saini makubaliano kuhusu ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Tanzania katika vyuo vikuu nchini Hungary kwa kipindi kingine cha miaka mitatu, kuanzia mwaka 2021 hadi 2023.

Makubaliano hayo yanatoa fursa kwa wanafunzi wa Tanzania kupata elimu katika vyuo vya Hungary kwa masomo ya shahada ya kwanza, shahada ya uzamili, na shahada ya uzamivu katika maeneo mbalimbali ya kitaaluma.

Makubaliano haya ni kielelezo kingine cha uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na nchi ya Hungary. Serikali ya Hungary imefurahishwa na muitikio wa Watanzania wanaoomba nafasi.

Kabla ya kutiliana Saini makubaliano hayo, kulikuwa na mazungumzo kuhusiana na namna ya kuimarisha Ushirikiano baina ya nchi zetu katika maeneo mengine, hususan yanayohusu biashara na uchumi.

Pia tarehe 8.12.2020, Obalozi wa Tanzania nchini Ujerumani ulifungua rasmi ofisi ya Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania iliyoko katika mji wa Brno, Jamhuri ya Czech.
 
Hivi karibuni, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ilimuidhinisha bwana Roman Grolig, kuwa Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania katika Jamhuri ya Czech. Kwa Tanzania, mji wa Brno ni mji wa kimkakati, kwani kila mwaka mamlaka za mji huo huandaa miongoni maonyesho makubwa ya biashara na utalii barani ulaya. Mji huo pia ni makao makuu ya Czech-Tanzania Chambers of commerce. 

Taasisi hiyo inatarajiwa kufungua ofisi mjini Dar es Salaam hivi karibuni, na katika miji mingine iliyoko Jamhuri ya Czech.

No comments: