KMC FC KUWAFUATA MTIBWA SUGAR YA MOROGORO KESHO



TIMU ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC kesho itaondoka jijini Dar es
Salaam kuelekea Mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo dhidi ya Mtibwa
Sugar utakaopigwa Ijumaa ya Disemba 11 katika uwanja wa Jamhuri
mkoani humo.

Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu John Simkoko pamoja na
msaidizi wake Habibu Kondo hadi sasa kimefanya maandalizi ya kutosha
na kwamba kipo tayari kwa mtanange huo na hivyo kuhakikisha kwamba
kinapata matokeo mazuri ili kuendelea kubaki katika nafasi nzuri ya
msimamo wa Ligi kuu Soka Tanzania Bara.

KMC FC ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika michezo yake miwili
mfululizo tangu kumalizika kwa mapumziko ya wiki mbili kupisha
michuano ya Kimataifa, imewahakikishia mashabiki na wapenzi waTimu
hiyo kuwa hivi sasa kila mechi imejipanga kupata matokeo mazuri.

Itakumbukwa kuwa KMC FC imewahi kupata matokeo mazuri katika michezo
mitatu ya ugenini ambayo ni dhidi ya Mwadui ambapo ilipata ushindi wa
magoli mawili kwa sifuri, mchezo dhidi ya Gwambia ilipata ushindi wa
magoli matatu kwa sifuri pamoja na mchezo dhidi ya Biashara iliyotoka
sare ya bao moja kwa moja

Imeelezwa kuwa hali ya kikosi ipo vizuri, na wamefanya maandalizi ya kutosha dhidi ya Mtibwa ipo na wanauhakika wakuchukua alama tatu muhimu ugenini.

No comments: