Madiwani wapya wilaya ya Mkuranga watakiwa kujikita kutatua kero na changamoto katika jamii

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga, Mhadisi Mshamu Munde (katikati)  akitoa muongozo wakati wa uzinduzi rasmi wa baraza hilo.(kushoto)Katibu Tawala Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Veronica Kinyemi kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga, Ali Msikamo.

KATIBU Tawala Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Veronica Kinyemi amempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa uteuzi wa Baraza la Mawaziri akiwemo Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega kuwa Naibu Waziri wa Habari, Sanaa utamaduni na Michezo.

Akifungua kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani kwenye ukumbi wa Flex Garden Mkuranga jana aliwapongeza wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga wakiongozwa na Mkurugenzi wao Mhandisi Mshamu Munde kuendelea kushirikiana vema na vyombo vya Ulinzi kuhakikisha hali ya usalama inakuwa shwari.

Kinyemi bila ya kumung’unya maneno aliwageukia Madiwani hao wapya na kuwataka wajikite katika kutatua kero na changamoto mbalimbali kwenye Sekta ya Elimu, Afya na Miundo mbinu kwa ushirikiano mkubwa ili kuleta tija ndani ya kipindi chao cha uongozi.

Akizungumzia Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri na Makamu wake Kinyemi aliwataka Madiwani kuchagua walengwa wenye maslahi mapana kwa wananchi wa Mkuranga na Halmashauri kwa ujumla na siyo kuchagua bora kiongozi.

Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya Mohamedi Mwela amemhakikishia Mkuu wa Wilaya kuwa watatumia vikao vyao vya kisheria zikiwemo Kamati za Kudumu ili kuyapa nguvu maagizo yote  ya kitaifa ambayo ni sawa na sheria ambayo ni pamoja na kufanya mazoezi mara mbili kwa mwezi sambamba na kufanya usafi wa kila mwisho wa mwezi.

Kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri na Makamu wake pamoja na kuundwa kwa kamati za kudumu na kupata wenyeviti wa Kamati hizo Madiwani wote (25) wa Kata na wale wa viti maalum (8) walikula kiapo cha utii na tamko la maadili.

Madiwani walimchagua Mohamedi Mwela Diwani wa Kata ya Mkuranga kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kura 33 kati ya 35 na kumchagua kambwili Diwani wa Kata ya Shungubweni kuwa makamu Mwenyekiti kwa kura 34 kati ya 35
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga, Mhadisi Mshamu Munde (kulia)akiteta jambo na Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya Mohamedi Mwela.

Baadhi ya viongozi mblimbli akifuatilia




Baadhi ya madiwani wakiapa.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga, Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdalah  Ulega na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga, Mhadisi Mshamu Munde wakiwapongeza madiwani baada ya kumaliza kula kiapo.

(Picha zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

No comments: