GSM yazindua shindano kuimarisha maisha ya watanzania
Afisa Mkuu wa Biashara wa kampuni ya GSM Group, Bw Allan Chonjo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa shindano la ‘Shinda na ung’arishe nyumba yako’ na ‘jishindie safari ya utalii ngorongoro’ linaloratibiwa na kampuni hiyo kuelekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Aliyeketi upande wa kulia ni Mratibu wa Masoko kutoka GSM Retailer, Bi Fatma Farah na kushoto ni Mratibu wa Masoko kutoka GSM Home, Bw Smart Deus.
===== ===== ========
. Kampuni ya uuzaji wa samani za nyumbani na ofisini pamoja na mavazi ya GSM imezindua shindano jipya la ‘Shinda na ung’arishe nyumba yako’ pamoja na jishindie safari ya utalii Ngorongoro yenye lengo la kutoa nafasi kwa Wateja na wadau wake kujishindia samani pamoja na nguo mbalimbali katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.
Akizungumzia shindano hilo mara baada ya hafla ya uzinduzi huo uliofanyika rasmi eneo la Mlimani City, jijini Dar es Salaam, Afisa wa Biashara wa GSM Group, Bw Allan Chonjo amesema kuwa, Lengo mahususi la kuanzisha shindano hili ni kutoa nafasi kwa wateja wote waliopo na wapya kuweza kujishindia zawadi kabambe watakazozifurahia wakati wa msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.
“Mwaka 2020 umekuwa na changamoto nyingi hususani mlipuko wa COVID-19 ambao uliathiri shughuli mbambali za kijamii na hata kuharibu mipango na malengo ambayo watu walikuwa wamejiwekea. Kwa kulitambua hilo sisi GSM tukaona hatuna budi kuanzisha shindano hili ili kila mmoja aweze kupata nafasi ya kujishindia bidhaa aliyokuwa akiitamani kuimiliki kutoka GSM Home and GSM Retail ,” Alisema, Afisa Mkuu wa GSM Group, Allan Chonjo.
Shindano hili litahusisha makampuni mawili ndani ya GSM kwa maana ya GSM Home ambayo ni wauzaji wa Samani za nyumbani na ofisini pamoja na GSM Retail ambao ni wauzaji wa Mavazi chini ya chapa ya SPLASH, BabyShop, Shoexpress, ANTA, Max na HomeBox ambayo pia wanauza vifaa vya nyumbani
Shindano hilo lililoanza rasmi tarehe mosi mwezi Disemba linatarajiwa kufanyika kwa awamu nne ambapo katika kila awamu, mshindi atapatiwa zawadi maalum kutoka GSM Home au GSM Retail.“Katika shindano hili kila mwananchi anafursa ya kushiriki kwa kujipatia kuponi ya ushiriki baada ya kununua bidhaa yoyote ya GSM Home yenye thamani kuanzia milioni 01 na kuendelea na kuweza kuingia kwenye droo itakayompa nafasi ya kujishindia zawadi mbali mbali, zawadi kubwa ikiwa ni kubadilisha muonekano wa nyumba yako,” alisema Mratibu Masoko wa GSM Home , Bw Smart Deus.
Na kwa upande wa mavazi, mteja akinunua nguo za thamani ya zaidi ya sh 50,000 kwa mara moja ataingia kwenye droo ya kujipatia zawadi mbalimbali zikwemo vocha za thamani ya shilingi kuanzia 250,000 au zawadi kubwa ya kulipiwa safari ya kwenda kutalii Ngorongoro kwa watu wawili.” Alisema Mratibu wa masoko wa GSM Retail, Bw Malick Mosha
“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa tunaendelea kuwa wauzaji na watoaji wa huduma bora ili kuyafikia mahitaji na kuboresha maisha ya watanzania hapa nchini kwa bei na nafuu na ubora wa hali ya juu.” Aliongeza, Allan Chonjo.
Kwa upande mwingine Safari hizi zimeratibiwa na kampuni ya GSM Travel ambao ni wabobezi kwenye kuandaa safari za ndani pamoja na za nje.
Maduka Yetu yanapatikana Dar es Salaam, Arusha pamoja na Dodoma kwenye maeneo yafuatayo;
Dar es Salaam: Mlimani City, GSM Msasani Mall, GSM Pugu Mall, GSM Home Mikocheni, Aura Mall,
Arusha: Jengo la TFA,
Dodoma: Shoppers Plaza pamoja na Capital City Mall
Kwa maelezo zaidi wasiliana na
Allan Chonjo – Afisa Biashara Mkuu
+255658450010
No comments: