BENKI YA STANBIC YATWAA TUZO YA BENKI BORA MWAKA 2020

 

 

Jarida la The Banker, limeitangaza benki ya Stanbic Tanzania Kama “Benki Bora Tanzania 2020”. Wakati wa kuchagua mshindi, jopo la majaji liliangalia jinsi benki zimejikita katika kutimiza mahitaji ya wateja na kuwa thabiti katika kipindi cha janga la ugonjwa wa Covid-19.

Miongoni mwao ni benki ya Stanbic ambayo ilifanya mambo mbali mbali ikiwemo kuairisha ulipaji wa mikopo ndani ya miezi mitatu hadi sita, na kuzindua huduma ya  Africa China Agency Proposition (ACAP) ili kuwezesha biashara za wateja wao kuendelea.

Akizungumzia tuzo hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Stanbic, Kevin Wingfield alisema; ”tunafuraha kupokea tuzo hii, napenda kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kuwa pamoja nasi hasa katika mwaka huu wenye changamoto mbali mbali, bila wao tusinge twaa tuzo hii. Pia nawashukuru wafanyakazi wetu ambao wamejikita katika kuhakikisha tunaendelea kutoa huduma bora.”

Mwaka huu benki ya Stanbic ilizindua kauli mbiu mpya - “inawezekana” kwa lengo la kuhamasisha imani katika maendeleo nchini Tanzania, huku wakiendelea kutoa huduma bunifu kulingana na mahitaji ya wateja wao. “Wateja wetu ndio kiini cha kila tunachokifanya, na mtazamo wetu mwaka huu ulilenga kujenga mahusiano mazuri na wateja na kuelewa mahitaji na ndoto zao.” aliongeza Wingfield.

Benki  hii imepokea tuzo nyingi kwa miaka mingi ikiwemo Benki bora ya uwekezaji mnamo mwezi Oktoba mwaka huu. “Hizi tuzo ni kielelezo cha juhudi zetu katika kuchangia maendeleo ya Tanzania na wateja wetu, hasa mabadiliko ya kiuchumi, ukizingatia mwaka huu tunasherehekea miaka 25 ya uwepo wa benki ya Stanbic nchini Tanzania” aliongezea Wingfield.

Benki ya Stanbic ni sehemu ya Standard Bank Group ambayo ni Benki kubwa Afrika kwa umiliki wa mali na inapatikana katika masoko 20 barani kote.

No comments: