WANAWAKE WAMPONGEZA RAIS DK MAGUFULI KWA NAMNA ALIVYOWAPA NAFASI ZA KIUONGOZI KWENYE SERIKALI YAKE
Charles James, Michuzi TV
WANAWAKE Viongozi kutoka Vyama mbalimbali vya siasa vyenye usajili wa kudumu nchini (ULINGO) vimempongeza Rais Dk John Magufuli kwa namna ambavyo amekua mstari wa mbele kuwaamini wanawake na kuwapa nafasi za kiuongozi.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo, Mratibu wa Ulingo, Saum Masjid amesema kitendo cha Rais Magufuli kuwapongeza wanawake viongozi kwenye hotuba yake wakati akizindua Bunge kimeonesha jinsi gani amekua mstari wa mbele kuwainua wanawake.
Saumu amesema ndani ya miaka mitano iliyopita serikali ya Dk Magufuli imewapa nafasi wanawake ambao kwa kiasi kikubwa anaamini wamekua na mchango kwa Rais katika kuwatumikia watanzania na kufikia mafanikio makubwa ya kiuchumi.
" Kwa mara ya kwanza katika historia ya Nchi yetu tumeshuhudia chini ya Dk Magufuli tukipata Makamu wa Rais Mwanamke ambaye kwa hakika amefanya kazi kubwa ya kumsaidia Rais katika kuwatumikia watanzania.
Tumeona pia Naibu Spika akishinda tena kiti chake hicho lakini safari hii akiwa siyo Mbunge wa kuteuliwa bali mbunge wa jimbo la Mbeya, ni matumaini yetu kama ambavyo katika kipindi chake cha kwanza alituamini wanawake basi na kipindi hiki pia aendelee kutuamini," Amesema Saumu.
Akizungumzia hotuba ya Rais, Saumu amesema ni hotuba iliyobeba dira ya Nchi kwa miaka mitano ijayo ikilenga kuwainua watanzania kwenye kila nyanj ya kiuchumi ikiwemo uvuvi ambapo Rais alisema serikali itaagiza meli nane za uvivu pamoja na kilimo ambapo ndege ya mizigo pia imeagizwa.
" Kwa kweli ni hotuba nzuri inayoakisi maana halisi ya kiongozi wa Nchi, niwaombe wakina mama tuendelee kumuunga mkono Rais wetu na kumuombea ili Mwenyezi Mungu azidi kumpatia afya njema ana atuletee maendeleo sisi wananchi, " Amesema Saumu.
Katibu wa Chama cha Viziwi Mkoani Dodoma, Amina Issa akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo.
No comments: