MO DEWJI AFUNGUKA ISHU YA CHAMA, ASEMA NI WA SIMBA
*Aeleza walivyojipanga kutetea ubingwa Ligi Kuu Tanzania Bara
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
SASA iwe rasmi Chama ni wa Simba!Hiyo ndio kauli ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba Mohamed Dewj wakati anatoa msimamo wa klabu hiyo kuhusu mchezaji wao machachari Cletus Chota Chama.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mo pamoja na mambo mengine yanayohusu klabu ya Simba ametumia muda mwingi kumuelezea Chama na hasa kuhusu usajili wake na hatma yake ndani ya Klabu ya Simba.
Akifafanua zaidi Mo amesema hivi " kumekuwa na kelele nyingi sana kuhusu Chama mara Kagere mara mchezaji huyo lakini Simba tumejipanga, unajua sisi hatufanyi vitu ambavyo tunakuja kujuta wakati mambo yameharibika, sisi tunakuwa mbele.Kwa hiyo wana habari kwamba Chama ameenda pengine, Chama hajaenda kokote.
"Fatiha naomba anisikilize nimeona ujumbe wake kuhusu Chama, naomba niseme Chama tumeshasaini naye mkataba, hii mambo anakwenda Yanga sio kweli, ukweli ni Chama tumeshamsaini na atabaki Simba hadi msimu wa mwaka 22.Anamisimu miwili na nusu. Kwa hiyo hii ishu ya Chama tuimalize hapa, mimi kama Mwenyekiti sijawahi kuja mbele ya waandishi wa habari kuzunguza mambo ya uongo. Nimeshawahi kusema uongo?
"Tumemalizana na Chama, hivyo Chama ni mchezaji halali wa Simba, ana miaka miwili na nusu, kwa hiyo nimeeleza haya wana Simba kwasababu kila nikienda mahali wanachama wanasema Chama asiondoke Simba , Chama asiondoke , kwa hiyo leo iwe rasmi Chama yupo simba,"amesema Mo.
Ameongeza ingawa kuanzia wiki ijayo watakuwa wakitipa mabomu mengine katika mitandao yao ya kijamii, na watakuwa wakiweka habari nyingi mpya, watu watashtuka kwasababu hata wale ambao wanasema wameondoka kumbe bado wako Simba.
"Chama bado ana mapenzi na Simba na wana Simba , viongozi na mashabiki tuna mapenzi naye, ni mchezaji mzuri , amekuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu, ameshinda tuzo tano, kwa hiyo sisi tuliona hilo na umhimu wake, ni mchezaji ambaye ameshafahamu mazin
gira na falsafa ya Simba, kwa hivyo tumeona hatuwezi kuruhusu watu kutuwahi na kumsajili .Kwa hiyo Chama ni mchezaji wa Simba Sports Club.
Aidha ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba imekutana siku ya jana na kuzungumza mambo mengi na kwamba wamejipanga na wamekuwa na kamati mbalimbali."Lakini siku hizi tumeona kumekuwepo na propaganda za uongo ambazo zinaendelea , unajua mwisho ya yote ukweli utonekana.
"Kuna gazeti nimesoma Chama ameshavaa jezi ya Yanga kabisa, kwa hiyo hii kitu unaweza kupelekwa mahakamani, kwa hiyo tusiende na romasi, vitu vinavyoengelewa barabara au na viongozi ambao labda wanajaribu kupotosha ukweli, sisi Simba hatuwezi kuropoka hovyo, siku tukisema na kweli linatokea , ishu ya Chama mambo yamekwisha.
Wakati huo huo, Mo amemzungumzia mchezaji wa Gerson Fraga ambaye amekuwa majeruhi ambapo amesema atachukua muda mrefu kupona, hivyo wamekubaliana kusajili mchezaji mwingine kujaza nafasi yake.
"Kwa bahati mbaya mchezaji wetu Fraga raia wa Brazili ameumia na atakuwa nje kwa muda mrefu, kwa hivyo kwenye dirisha dogo hili kwa mapendekezo ya Kocha tutajaribu kumtafuta mchezaji mwingine ili kuziba hiyo nafasi,"amesema Mo.
No comments: