VITUO VYA MALEZI KWA WATOTO WADOGO VYAPONGEZWA
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii), Dkt. John Jingu akiwa amembeba mtoto Raphael wakati alipotembelea Kituo cha Kulelea Watoto wadogo Mgolole kilichoko eneo la Bigwa Mkoani Morogoro. Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii), Dkt. John Jingu akimpa zawadi ya maziwa ya kopo mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Kulelea Watoto wadogo Mgolole kilichopo Mkoani Morogoro.
Msimamizi Kituo cha Kulelea Watoto wadogo Mgolole kilichopo Mkoani Morogoro Sr. Everista Bunga akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii), Dkt. John Jingu (kushoto) alipotembelea kituo hicho. Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii), Dkt. John Jingu akipokelewa kwa wimbo na watoto wanaolelewa na Kituo cha Kulelea Watoto wadogo Mgolole kilichopo Mkoani Morogoro.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
*****************************************
Na Mwandishi Wetu Morogoro
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii), Dkt. John Jingu amevipongeza vituo vinavyohusika na malezi kwa watoto kutokana na kazi kubwa wanayoifanya kwa taifa.
Dkt. Jingu ameyasema hayo Mjini Morogoro wakati alipotembelea Kituo cha Kulelea Watoto wadogo cha Mgolole kinachoendeshwa na Kanisa Katoliki.
Dkt. Jingu amesema kazi ya kulea watoto wasio na na wazazi au walezi kutokana na sababu mbalimbali ni kubwa na inahitaji nguvu ya pamoja kutoka kwa jamii ili kufanikisha lengo la malezi bora kwa watoto.
Akitoa mfano kwa watoto 52 wanaolelewa katika kituo Mgolole, Katibu Mkuu Dkt. Jingu amesema walezi wanafanya kazi kubwa kuhakikisha watoto hao wanakuwa katika mazingira salama.
Amefafanua kuwa suala la malezi ni muhimu sana katika kuhakikisha tunajenga taifa lenye watu wenye maadili na uzalendo kwa nchi yao.
“Unaweza utakuta familia ina watoto watatu tu lakini suala la malezi linakuwa gumu ila ninyi mna watoto 52 na mnaweza. Hili mnalolifanya ni ibada katika Imani zetu zote na ninawapongenza sana kwa hili” alisema.
Hata hivyo, Katibu Mkuu amesisitiza kuwa Vituo hivyo lazima visajiliwe ili kutambulika na Serikali na wadau wengine ili kiweze kufanya kazi zao katika mazingira mazuri.
Kwa upande wake, Msimamizi wa Kituo cha Kulelea Watoto wadogo Mgolole Sr. Everista Bunga ameishukuru Serikali kwa kuvisimamia vituo hivyo na kuviongoza katika masula ya uendeshaji ma utoaji wa elimu ya malezi kwa watoto.
“Watoto wanaolelewa katika kituo cha Mgolole wamepatikana kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kufiwa na mama zao, kutupwa na wazazi, kuzaliwa na wazazi wenye magonjwa mbalimbali yanayowakosesha wazazi uwezo wa kuwalea watoto” alisema
No comments: