STARTIMES YAFANYA UZINDUZI WA KAMPENI YA MSIMU WA SIKUKUU “PESA KIDOGO TU”
Kampuni ya Star Media (T) Limited kupitia chapa yake ya StarTimes imezinduzi Kampeni yake katika msimu huu wa sikukuu, iitwayo “PESA KIDOGO TU”.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa StarTimes Bw. David Malisa amesema Kampuni hiyo imeona ni vyema kwa Wateja wake kupata kutazama maudhui mbalimbali pamoja na kupata bidhaa za Kampuni hiyo kwa PESA KIDOGO TU, wateja wataweza kutazama Tamthilia kama Gangaa, Mashindano ya kusaka Vipaji yani BSS, kupitia chaneli pendwa ya ST Swahili bila kusahau ligi za Laliga na Europa zinazoendelea kurindima ndani ya Chaneli za michezo na maudhui mengine mengi.
Malisa amesema kuwa Kampuni hiyo ina bidhaa mbalimbali ikiwemo Kisimbuzi chake chenye vifurushi mbalimbali vinavyokidhi mahitaji ya kila lika na kwa gharama nafuu, amesema ukinunua Set ya Dish kwa Shilingi 69,000 unapewa kifurushi cha juu cha mwezi BUREE!.
"Na endapo utanunua Seti ya Antenna kwa Shilingi 49,000 Tu!utapata pia kifurushi cha juu cha mwezi BUREE,mbali na hiyo kuna kubwa kuliko,ukiwa na App ya Startimes On utaweza kuunganisha mpaka watu watatu kupitia kisimbuzi cha StarTimes na kuangalia maudhui ya Starimes", amesema Malisa
StarTimes imewahakikishia wateja wake kuwapa kile kilicho bora, kwa kufunga mwaka na PESA KIDOGO TU! "Muhimu zaidi lipia leo hii kifurushi cha uhuru Tsh 20,000 tu ikiwa mtumiaji wa kisimbuzi cha antenna ama Kifurushi cha smart Tsh 21,000 tu ikiwa mtumiaji wa kisimbuzi cha dish,tunawatakia maandalizi mema ya sikukuu na muendelee kufurahia huduma zetu,mkumbuke tupo kwa ajili yenu", ameongeza Malisa.
Meneja Masoko wa StarTimes Bw. David Malisa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampuni hiyo kuanzisha Kampeni yake katika msimu huu wa sikukuu, iitwayo “PESA KIDOGO TU” leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Pendo Mango na kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja wa StarTimes, Deusdedit Manungulile.
Msimamizi wa mitandao ya kijamii wa Staritimes Mrisho Selemani(wa pili kushoto) akionesha hatua za kujiunga na huduma ya StarTimes App itakayowezesha watmiaji wa Startimes kutazama kwenye simu zao za mkononi. Wa pili kulia ni Meneja Masoko wa StarTimes, David Malisa, wa kwanza kulia ni meneja Uhusiano wa Startimes, Pendo Mango.
Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja wa StarTimes, Deusdedit Manungulile akizungumzia kuhusu huduma wanazozitoa hasa kwenye kipindi hiki cha Sikukuu wakati wa uzinduzi wa kampeini ya "PESA KIDOGO TU" leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Masoko wa StarTimes Bw. David Malisa na kushoto ni Msimamizi wa mitandao ya kijamii wa Staritimes Mrisho Selemani.
No comments: