TECNO CAMON 16 KUJA KUWAPINDUA WAPINZANI WAKE

Ni wazi kuwa katika ulimwengu wa simu janja watumiaji hawaridhiki tena na sura nzuri ya simu pekee, Mchanganyiko wa muonekano, pamoja na kazi ambazo simu huweza kufanya imekuwa sababu kubwa ya kuamua simu gani ya kununua. Hata hivyo, "uwezo wa kamera" kwa simu janja sasa imekuwa ni msamiati unaotumiwa sana katika tasnia hii. Kampuni nyingi za simu janja hushindana kwa bidii ili kuwa simu bora yenye sifa nzuri lakini pia yenye uwezo mkubwa wa kupiga picha.

Hivi karibuni, kampuni nyingi zimezindua bidhaa zao mpya za simu janja, kama vile OPPO, TECNO (https://ift.tt/3gZFVoS), Samsung, Huawei, Vivo, Realme, Xiaomi na zingine, na hii imesadia kuwapa vijana wa leo chaguzi zaidi. Wakati huu tulichagua simu nne za hivi karibuni za Android kufanya ulinganisho na kujua ni nini kinacho fanya kazi kwa ubora Zaidi kwenye simu hizo. Simu hizo ni Pamoja na TECNO CAMON 16 Premier, Samsung A51, Huawei Y9, na OPPO A9.

Uwezo wa kamera - kamera za mbele na nyuma

Ni ukweli usio pingika kuwa simu bora kuliko zote sokoni ni lazima iwe na kamera bora, na hapa ndipo inapokuja TECNO CAMON 16 Premier e, simu hii inakuja na kamera kuu ya Megapixel 64 MP, wakati Samsung A51 na OPPO A9 zinakuja na kamera ya kuu za hadi megapixel 48MP, huku Huawei Y9 ikiwa na kamera kuu ya 24MP. 

Mbali ya hayo, TECNO CAMON 16 Primer ina kamera ya mbele ya 48MP, wakati Samsung A51 inakuja na kamera ya mbele ya 32MP, OPPO A9 na Huawei Y9 zote zinakuja na kamera za Megapixel 16 MP. Mlinganisho huo unaonyesha wazi kuwa picha zinazopigwa na TECNO Camon Premier zitakuwa na mwanga zaidi na hivyo zitakuwa na ubora kuliko picha zinazopigwa na simu nyingine hapo juu.

Ikiwa wewe ni mpenzi wa picha, au unatumia simu kupiga picha kwenye matukio muhimu, TECNO CAMON 16 Premier lazima itakufaa sana. Lakini pia, kama wewe ni mpenzi wa selfie, TECNO CAMON 16 Premier inakuja na kamera ya Megapixel 48 ambayo itakusaidia kupiga picha nzuri na angavu, Pia kama wewe unapenda kushiriki nyakati nzuri na marafiki au ndugu na jamaa, Camon 16 Premier inakuja na kamera ya mbele ya ziada yenye Megapixel 8 ambayo itakusaidia kuchukua picha zako ukiwa na ndugu na jamaa kwa urahisi Zaidi (Group Photo).

Uwezo huo mkubwa wa kupiga picha unawezeshwa na processor yenye nguvu ya Mediatek MTK G90T ambayo imetumika kwenye simu hii ya Camon 16 Premier. Processor hii inaipa nguvu simu ya Camon 16 Primier hadi kufikiwa 2.05GHz.

Bila kujali kama ni usiku au mchana ni wazi kuwa kupata picha bora imekuwa ni jambo la muhimi, TECNO CAMON 16 Premier inakuja na teknolojia ya Super HIS na EIS+AIS, na wakati huohuo simu hii pia inakuja na teknolojia ya HIS hybrid intelligent anti-shake technology. Teknolojia zote hizi zinakusaidia kupiga picha vizuri wakati wa usiku ikiwa Pamoja na kuchukua video ambazo ni bora Zaidi bila kuwa na mitetemeko kwenye video hata kama unachuku video huku unatembea.

Mbali na teknolojia hiyo, TECNO CAMON 16 Premier inakuja na teknolojia inayo kuwezesha kuchukua video za taratibu au Slow Motion hadi kufikia kiwango cha fremu 960. Hii yote inawezekana kutokana na simu hii kuwa na uwezo mkubwa wa processor Pamoja na RAM ya GB 8 ambayo ndio hufanya kazi hii kuwa rahisi Zaidi.

Battery

Simu kuwa na battery yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa muda mrefu imekuwa ni jambo la muhimu miongoni mwa watumiaji wa simu janja. TECNO CAMON 16 Premier inakuja na battery yenye uwezo wa 4500mAh ambayo pia inakuja na teknolojia ya quick charge ambayo inaweza kuchaji battery hiyo hadi asilimia 70 kwa muda wa dakika 30.

Huu ni uwezo mkubwa sana ukilinganisha na simu za Huawei Y9 na Samsung A51 ambazo zinakuja na battery ya 4000mAh. Japokuwa Oppo A9 inayo battery kubwa ya 5000mAh, ni wazi kuwa teknolojia ya Quick charge ya TECNO CAMON 16 Premier ni bora Zaidi na salama hasa ukizingatia simu hii inakuja na teknolojia ya kuzuia simu hii kupata joto kwa haraka hasa inapokuwa inachaji kwa kutumia teknolojia ya Quick Charge. 

Kioo

TECNO CAMON 16 Premier inachukua taji pale linapo kuja swala la kioo, Simu hii inakuja na kioo kikubwa cha inch 6.85, kioo ambacho kinafaa Zaidi kwa wapenzi wa kucheza game kwenye simu, Pamoja wapenzi wa kuangalia filamu na tamthilia kwenye simu. Tofauti na simu nyingine kama Samsung A51 na OPPO A9. Camon 16 Premier inakuja na kioo chenye resolution ya 90Hz ultra-clear resolution ambayo inafanya kioo cha simu hii kuwa angavu na chenye kuonyesha rangi halisi na kufanya kazi kwa haraka Zaidi.

Kwa sababu ya hii, TECNO CAMON 16 Premier imehamisha sehemu ya ulinzi ya fingerprint kutoka chini ya kioo na sasa sehemu hii inapatikana kwa pembeni mwa simu hii. Hii inafanya kuwa rahisi Zaidi kufungua simu yako hata kama umeshika simu yako kwa mkono mmoja.

Hitimisho

Baada ya kulinganisha simu hizo zote kwenye mambo yote hayo ni wazi kuwa, TECNO CAMON 16 Premier ni simu bora na tofauti kati ya simu hizo nne. Simu hii inakuja na sifa zote ambazo mtumiaji makini angetamani kuzipata, ikiwa Pamoja na uwezo bora wa kudumu na chaji, kamera nzuri, kioo bora chenye kuonyesha rangi angavu, Pamoja na muundo mzuri wa kisasa, ni wazi kuwa simu hii inakuja na teknoloijia bora na sifa bora kwa gharama nafuu sana kuliko simu zote hapo juu. 



No comments: