NIDHAMU, BIDII VYA MBEBA MOBETO 2020
Na Khadija seif, Michuzi TV
KATIKA wasichana wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya Bongofleva kwa sasa huwezi kuacha kumtaja Hamisa Mobeto.
Mlimbwende huyo amekua akifanya vizuri kwa upande wa muziki pamoja na tasnia ya bongomovie kwa sasa, ambapo pia amekua akiendesha kazi zake za ubunifu wa mavazi.
Mobeto amekua akiramba dili tofauti tofauti katika makampuni kutokana na bidii yake kwenye kazi zake ikiwa ni kielelezo tosha cha kufanya uaminifu miongo mwa kampuni ambazo zimekua zikimpa ubalozi.
Kwa upande wa kampuni ya utengenezaji wa taulo za kike human cherish(HQ) wamempa ubalozi hamisa Mobeto kwa ajili ya kuitangaza bidhaa hiyo.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo Celine amesema kampuni hiyo ina imani na Hamisa Mobeto na imeamua kumpa ubalozi ili aendelee kufikisha bidhaa hiyo karibu na watumiaji na waendelee kuiamini.
"Mobeto ni msichana ambae anajielewa na kujitambua, nidhamu yake ndio kitu pekee kilichofanya tumpe ubalozi huo wa kutangaza bidhaa yetu ya taulo za kike."
Hata hivyo ameeleza kuwa sababu kubwa ya kumchagua hamisa na sio watu wengine.
"Tulifatilia mienendo yake kwa kipindi kirefu tukaona ni sahihi kumpa nafasi hiyo japo makosa madogo madogo kila binadamu anayo hivyo inaeleweka tu."
Nae Hamisa Mobeto hakusita kushukuru kampuni hiyo nakusema ataendeleza gurudumu la kusongesha kampuni hiyo na kuwatangazia watumiaji wa bidhaa hiyo kuwa mazuri mengi yanakuja.
"Nina furaha Sana kuona bidii yangu kwenye kazi zangu inaendelea kunifanya wa thamani Sana machoni mwa watu na kuamini kunipa baadhi ya majukumu." Hamisa
Hata hivyo Mobeto ameeleza kuwa kampuni hiyo imekua ikirudisha fadhira kwa jamii na Safari hii wameamua kutengeneza taulo kwa ajili ya wasichana wadogo kabisa kwa bei nafuu kwa ajili ya mashuleni.
"Kwakua tayari nimeshapewa ubalozi kwa muda ambao ni endelevu hivyo napenda kuchukua nafasi hii kuwajulisha kuwa taulo mpya tumezindua kwa ajili ya wasichana ambao Mara nyingi wamekua wakikosa kuhudhuria vipindi madarasani kutokana na kukosa kukidhi bei ya taulo za kujistiri hivyo hii mpya itaweza kufanya wamudu kununua na itakua inapatikana shuleni tu." Amesema Hamisa
No comments: