WANACHAMA WAPYA ZAIDI YA AROBIAN WAJIUNGA NA CCM

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akipokea kadi za vyama mbalimbali vya upinzani kutoka kwa wanachama zaidi ya arobainI  wa vyama hivyo wa kata ya Kimanzichana walioamua kuvihama na kujiunga na CCM katika mkutano wa kampeni wa kuomba kura wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega  akionesha kadi za vyama mbalimbali vya upinzani kutoka kwa wanachama zaidi ya Arobiani  wa vyama hivyo wa kata ya Kimanzichana walioamua kuvihama  na kujiunga na CCM katika mkutano wa kampeni wa kumuombea kura mgombea urais wa CCM, Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mbunge na Diwani wa CCM kwenye kituo cha Mabasi Ulega wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
(Picha na Emmanuel Massaka michuzi Tv)
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega  akiwaomba kura wananchi wa Kimanzichana wawampigie kura wagombea  CCM  katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye kituo cha mabasi Ulega, ambapo ameahidi kusimamia uboreshaji wa huduma za elimu na afya.
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega.

No comments: