KMC FC YAZITAKA ALAMA TATU ZA YANGA KESHO UWANJA WA CCM KIRUMBA MWANZA

 


……………………………………………………………………

Na.Mwandishi Wetu,Mwanza

Kocha wa Timu ya Manispaa ya Kinondoni KMC FC Habibu Kondo amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kwa mpambano wa kesho dhidi ya Yanga na kwamba anaimani ataibuka na ushindi mnono katika mchezo wa Ligi kuu soka Tanzania Bara.

Habibu amesema kuwa hadi Sasa ameshafanya maandalizi ya kutosha na kwamba hanahofu na mchezo huo kwakuwa anakikosi kipana na kwamba silaha alizonazo zinatosha kuiadhibu Yanga katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Ameongeza kuwa licha ya kwamba kikosi hicho hakikuweza kufanya vizuri katika michezo kadhaa iliyopita lakini tayari ameshazifanyia kazi changamoto zilizopelekea kupoteza kwa michezo hiyo.
” Tumekuja mwanza kutafuta alama 9 katika michezo mitatu tuliyonayo, kesho tunachukua alama tatu kwa Yanga halafu tunaenda kuchukua kwa Gwambia, Biashara na hivyo tukirejea Jijini Dar es Salaam tunarudi kwa kishindo kutokana na ushindi ambao tutakuwa tumeupata” amesema Kocha Habibu.
KMC FC kesho inacheza mchezo wake wa mzunguko wa nane katika msimu wa Ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Yanga na kwamba kikosi chote kipoimara katika mpambano huo sambamba na wachezaji kuwa na morali nzuri ya mchezo.” ameongeza Kocha Habibu.
Wakati huo huo Afisa Habari na Mahusiano wa Timu hiyo ,Christina Mwagala amesema kuwa katika mchezo huo wamejipanga vizuri katika suala zima la uuzwaji wa Tiketi na kwamba hakutakuwa na changamoto zozote katika mchakato huo.
Ameongeza kuwa katika kuhakikisha kuwa mpambano huo unakuwa mzuri, uongozi umejipanga na kwamba mageti yote yatakuwa wazi kuanzia saa 1.00 asubuhi na hivyo kila geti litakuwa na wahusika wanaokata Tiketi hizo.

No comments: