UMMY MWALIMU -NITAMALIZA MIGOGORO YA ARDHI JIJINI TANGA

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akizungumza na wananchi wa Kata ya Usagara Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni

KATIBU Mwenezi wa CCM wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapange akimuombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu
Msanii wa mziki wa Bongofleva Kassim Mganga akiwasha moto kwenye mkutano huo

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amesema endapo atachaguliwa kuliongoza Jimbo hilo atahakikisha anamaliza migogoro ya ardhi iliyopo kwenye Jiji la Tanga ikiwemo Kata ya Usagara kwa kusimamia wenye haki kupata haki yao.
Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Usagara Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika mtaa wa Usagara Kijijini jirani na Magorofa ya Bandari.
Alisema kwamba anatambua kwenye Jiji hilo kuna baadhi ya maeneo kuna migogoro ambayo imekuwa ni kero kubwa kwa wananchi hivyo ataishughulikia kwa kuhakikisha anasimamia haki ili mwenye kustahili apate haki yake.
“Ndugu zangu wana Usagara ninafahamu ipo migogoro ya ardhi hapa kwenu lakini na Tanga kwa ujumla hivyo nipeni ridhaa ya kuwa mwakilishi wenu tuweze kushughulika nayo kuhakikisha tunaimaliza”Alisema
Mgombea huyo alisema anafahamu kuna changamoto ya migogoro ya ardhi katika kata ya Usagara ikiwemo Usagara Kijijini ambapo alisema kwenye hilo atalifanyia kazi sambamba na kufanya maboresho ya wakazi wa Usagara kijijini.
“Kuhusu suala la umiliki wa nyumba kwa watu walionunua Nyumba za TBA na TPA niliwahaidi wana Usagara nitumeni bungeni suala lenu nitalikamilisha “Alisema Ummy Mwalimu.
Hata hivyo alisema kwamba ataendelea kuboresha miundombinu ya shule ya Sekondari Usagara na Ujenzi wa barabara ya white rose ambayo hujaa maji wakati wa mvua.
No comments: