Mbio za NBC Marathon Zazinduliwa Rasmi Jijini Dar es Salaam
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Shirikisho la Riadha Taifa (RT) hii wamezindua rasmi mbio zinazofahamika kwa jina NBC Marathon, zinatarajiwa kufanyika Novemba 22 mwaka huu jijini Dodoma.
Pamoja kukuza mchezo huo nchini, mbio hizo pia zinalenga kuchochea mapambano dhidi ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi nchini, kwa mujibu wa waandaji hao.
Hafla ya uzinduzi wa mbio hizo imefanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wadau wa mchezo huo wakiwemo viongozi waaandamizi wa Baraza la michezo Tanzania (BMT), Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Maofisa waandamizi wa benki ya NBC pamoja na wawakilishi wa vyombo vya habari.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi alisema pamoja na dhamira ya dhati ya benki hiyo ya kuwekeza kwenye mchezo wa riadha kupitia mbio hizo, mapato yote yatokanayo na usajili wa wawamkibiaji katika mbio hizo yataelekezwa kwenye vita dhidi ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya uzazi kupitia Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
“Tumeamua kuelekeza nguvu zetu katika mapambano hayo tukitambua kwamba ugonjwa huu ndio unaoongoza kwa vifo vya saratani hapa nchini. Hivyo mbio hizi za NBC Dodoma Marathon itakuwa jukwaa zuri la kusambaza ufahamu juu ya ugonjwa huu ambao tunaambiwa kwamba ukiwahiwa unatibika.’’ Alisema.
Katika hafla hiyo pia ilishuhudiwa benki hiyo pamoja na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) wakisaini mkataba wenye thamani ya sh Milioni 300 ikiwa ni ufadhili wa benki hiyo katika ya kuendesha mbio hizo katika kipindi cha miaka mitano.
“Ni maono yetu kwamba NBC Dodoma Marathon ndio mbio ambayo itapeperusha jina la NBC katika miaka ijayo, na hivyo tunadhamiria kuendelea na mbio hii kwa kipindi cha miaka mitano.’’
“Zaidi ni matumaini yetu kwamba uwekezaji wetu kwenye mchezo wa riadha utatumika vizuri na hivyo kuleta mafanikio kwa wanariadha wetu na kwa nchi yetu kwa ujumla katika siku za usoni.,’’ aliongeza Bw Sabi
Usajili wa mbio hizo tayari umeanza kupitia matawi ya benki hiyo kote nchini sambamba na mitandao ya kijamii ya benki hiyo.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Bw Anthony Mtaka pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa kuamua kuwekeza kwenye kuinua mchezo huo nchini , alisema lengo ni kuifanya mbio hiyo kuwa ya mfano na yenye utambuzi wa kimataifa (International Recognition).
“NBC Dodoma Marathon itakuwa na mbio nne yaani 5km, 10km, 21km na 42km. Kwa kuwa lengo ni kuifanya itambulike kimataifa tumehakikisha kwamba njia zote zinapimwa na mpimaji anayetambulika na Shrikisho la Riadha la Dunia (World Athletics). Zoezi hilo la kupima lilikamilika tarehe 17 Oktoba 2020 jijini Dodoma. Kwa sasa tunasubiri vyeti kutoka Shrikisho la Riadha la Dunia kuthibitisha utambuzi huo.’’ Alibainisha.
Alisema uamuzi wa mbio hizo kufanyika jijini Dodoma ulizingitia sababu za msingi kadhaa ikiwemo mandhari ambayo ni kivutio kwa wakimbiaji, mpangilio wa barabara ambazo haziingiliani na barabara kuu na hivyo kuwa salama kwa wakimbiaji wa aina zote.
“Lakini pia tuliona jiji la Dodoma, kama mji wetu mkuu, unastahili kuwa na tukio kubwa la mchezo unaotambulika kimataifa. Kwa hiyo ni dhahiri kwamba uamuzi wetu wa kupeleka mbio hizi Dodoma ulikuwa sahihi.’’ Alisema.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dk Julius Mwaiselage pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa jitihada hizo huku akibainisha kuwa mbio hizo zitaongeza mwamko wa wana jamii kushiriki katika mazoezi hatua ambayo itasaidia miili yao kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (Katikati) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh mil 300 kwa Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Bw Anthony Mtaka ikiwa ni ufadhili wa benki hiyo kwa shirikisho hilo katika kipindi cha miaka mitano ikiwemo kuendesha mbio za NBC Marathon, zinatarajiwa kufanyika Novemba 22 mwaka huu jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dk Julius Mwaiselage (Kushoto).
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (Kushoto) akimkabidhi Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Bw Anthony Mtaka mkataba wenye thamani ya sh Milioni 300 ikiwa ni ufadhili wa benki hiyo kwa shirikisho hilo katika kipindi cha miaka mitano ikiwemo kuendesha mbio za NBC Marathon, zinatarajiwa kufanyika Novemba 22 mwaka huu jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wanaoshuhudia ni pamoja viongozi waandamizi wa RT.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (Kushoto) akizungumza kwenye hafla hiyo.
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Bw Anthony Mtaka (Kulia) akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dk Julius Mwaiselage (Kushoto) akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwanariadha mashuhuri wa zamani kutoka Tanzania Bw Juma Ikangaa akizungumza kwenye hafla hiyo.
Wadau wa mbio za NBC Marathon akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi ( katikati), Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Bw Anthony Mtaka (wa sita kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dk Julius Mwaiselage (wa tano kushoto)na viongozi waandamizi kutoka RT wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa hafla hiyo.
Wadau wa mbio za NBC Marathon akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa tatu kulia), Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Bw Anthony Mtaka (Katikati) , Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dk Julius Mwaiselage (wa nne kushoto wakiwa kwenye picha ya pamoja wanachama wa klabu ya wakimbiaji ya Wasafi wakati wa hafla hiyo.
Wadau wa mbio za NBC Marathon akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa tatu kulia), Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Bw Anthony Mtaka (wa tatu kushoto) , Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dk Julius Mwaiselage (wa pili kushoto), Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Neema Rose Singo (wa pili kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja waandishi wa michezo waandaamizi nchini Bw Bw Shafii Dauda kutoka Clouds Media Group(Kulia) na Maulid Kitenge kutoka Wasafi Media (Kushoto) wakati wa hafla hiyo.
Wadau wa mbio za NBC Marathon akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa tatu kulia), Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Bw Anthony Mtaka (wa tatu kushoto) , Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Dk Julius Mwaiselage (wa pili kushoto), Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Neema Rose Singo (wa pili kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja waandishi wa michezo waandaamizi nchini Bw Bw Evance Mhando kutoka TBC (Kushoto) na Ahmed Mohamed kutoka Azam Media wakati wa hafla hiyo.
No comments: