DK.JOHN MAGUFULI AUNGURUMA MANYARA, ASISITIZA AMANI ...AMANI...AMANI



*Awashangaa wanaogombea urais wa Tanzania halafu wanataka kuvunja muungano

*Asisitiza umuhimu wa kuchagua viongozi wataendelea uhuru wa kweli wa watanzania

*Asema wasaliti kama Yuda bado wapo nchini, wananchi wasikubali kudanganywa

Na Said Mwishehe, Michuzi TV -Manyara

MAELFU ya wananchi wa Mkoa wa Manyara wamejitokeza kwenye mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli ambaye pamoja na mambo mengine amewahimiza watanzania wote kuendelea kudumisha amani na tulivu huku akieleza wake ambao wanahubiri uvunjifu wa amani wanyimwe kura siku ya kupiga kura ambayo ni Oktoba 28 mwaka huu.

Akizungumza mbele ya wananchi hao leo Oktoba 25,2020 wakati akiomba kura ili achaguliwe tena kwa miaka mitano mingine aongoze nchini, Dk.Magufuli amefafanua kuwa wamedumisha  amani na utulivu na kwamba Tanzania imebaki kuwa nchi yenye amani na hakuna vurugu.

"Sisi watanzania nchi yetu ni amani, Manayara ni watu wenye amani, amani hii imejengwa tangu enzi za Mwalimu Nyerere, akaja mzee Alhasan Mwinyi, akaja Mzee Mkapa ambaye ametangulia mbele za haki hivi karibuni, kisha akaja mzee Jakaya Kikwete na sasa nimekuja mimi na nimeendeleza, niwaombe tuendelee kulinda amani ya nchi yetu.

"Kuna wagombea ambao wamekuwa wakihubiri uvunjifu wa amani kwa kuhamasisha fujo, wanawahamasisha vijana ambao wakiona mambo yameharibika  wanakimbia, vijana mtambue kabla ya kuwa vijana mlikuwa watoto na kuna siku mtakuwa wazee.Naomba tutunze amani yetu, vitabu vya dini zote vinazungumzia amani, na ninajua hata siku ya kupiga kura wamejipanga kufanya vurugu.

"Nimeikuta hii nchi ikiwa na amani na anataka kuiacha ikiwa na amani,maendeleo yamefanyika kwasaababu kuna amani, ukikosa amani hakuna ambacho kitafanyika, hivyo tuitunze amani yetu, nataka nchi iendelee kuwa kisiwa cha amani.Mwaka 2015 nilipofanya ziara ya kwanza kwa Rwanda  rafiki yangu Rais Paul Kagame akanikaribisha mahali ambapo watu waliuawa karibu milioni moja, pale Kigali,

"Kama umefika pale utajua maana ya amani, vichwa vimepangwa, kuna vichwa hadi vya watoto vimechomwa mkuki na kubaki pale, nampongeza Kagame amesimamia amani, alinipeleka nikajifunze kuhusu umuhimu wa amani, unaangalia mafuvu hadi unachanganyiwa.Kuna mifano mingi, kuna nchi zilikuwa na amani leo ni vita, ukichezea amani ni sawa na kuchezea yai, ukiliangusha huwezi kuliunganisha tena,"amesema Dk.Magufuli.

Amefafanua kuwa tunu ya ambayo imeachwa na waasisi wa Taifa hili ni ya amani na kwamba Siria mpaka leo wanapiga sio kwamba wanapenda, Libya wanapigana wakati waliowachanisha wanaiba mafuta.Nchi nyingi tajiri duniani zinachonganishwa ili watu wachukue mali."Mimi mlinichagua ili niwaambie ukweli na huu ndio ukweli, wapo wengine wana hati sa kusafiria nyingi nyingi tu, ninawaomba mjifunze historia ya maeneo mengine, msikubali kudanganywa, najua wasaliti wako wengi.

"Hata Yesu alisalitiwa, Yuda aliyekuwa mtunza hazina wake na bado akamgeuka, usidhani akina Yuda wameisha Tanzania bado wapo, na katika uchaguzi huu nimetukwana.Ninachotaka kuwambia amani tuliyano tusifikiri imejileta wenyewe,"amesema Dk.Magufuli mbele ya maelfu ya wananchi hao wa Manyara.Baba wa taifa alifanya kazi kubwa kupata Uhuru bila kumwaga damu, nchi nyingi sana zimemwaga damu na hata bendera zao ni damu.

"Hakuna Taifa ambalo limefanikiwa ndani ya mvurugano, halipo , tuilinde amani, unasikia mtu anazungumza nimeshinda, sisi CCM tuna wabunge 28 ambao wamepita bila kupingwa, ulizeni Chama kingine kama kuna mbunge amepita bila kupingwa, halafu mtu anasema nitashinda na asiposhinda anakwenda barabarani, aende na mkewe,"amefafanua.

Aidha Dk.Magufuli amesema wamedumisha uhuru wa nchi yetu kwani baada ya kupata uhuru wa taifa hili Baba wa Taifa alitamka tunataka kutengeneza taifa lenye uhuru wa ukweli na sio uhuru wa bendera,hivyo naye katika uongozi wake pamoja na waliomtangulia wamedumisha uhuru wa kweli wa nchi yetu.Amesema wakati wa janga la Corona alihakikisha analisimamia taifa na kubaki huru bila kuingiliwa na yoyote ile.

"Walitaka tuweke nchi lock down lakini nilikataa kwani siwezi kuiweka nchi kwenye lock down na katika kuzingatia uhuru wa kweli, tuliamua kusimama na Mungu katika kupambana na Corona, kwasababu niliamini ukiweka watu ndani watu wangekufa zaidi, nikaseme kwenye hili tunamtanguliza Mungu ambaye ndio jibu la watanzania wenye shida zote.Tulifunga na kumlilia Mungu, leo Tanzania ni nchi pekee ambayo haina Corona duniani.

"Tumshukuru Mungu, yamefanikiwa haya kwasbabu tulimtanguliza Mungu ambaye anaipenda Tanzania, mkiangalia televisheni mtaona huko kwenye mataifa mengine watu wanavyokufa,wanajiuliza watanzania wana damu gani?Watanzania wana damu ya Mungu.Wako watanzania waliokuwa Ulaya na walizunguka na kuiambia dunia kwamba Tanzania kuna Corona, hata waliokuwa bungeni nao waliamua kutoka bungeni, kwao maisha yao na sio watanzania.

"Mwaka huu waoneshwe hadharani kwa kuwanyima kura, wajue hawana kitu mwaka huu, hawataki kusema hadharani Mungu anaweza, wameshindwa kutubu mbele ya wananchi wao na kushindwa kuwaomba msamaha kutokana na kauli zao na matando yao wakati watanzania wakipambbana na janga hilo.Tanzania iko safi na hii ndio dhana ya kudumisha uhuru, hatukukubali kupewa masharti, wananchi hakikisheni mnachagua mtu wa kutunza tunu zetu, na mimi nina sifa zote,"amesema Dk.Magufuli.

Pia amezungumza umuhimu wa kulinda Muungano uliopo nchini ambao umefikisha miaka 57 tangu ulipoanzishwa kutokana na mataifa mawili huru yaliyoungana na kupata Tanzania."Hata hivyo kuna wagombea wamejitokeza wanasema wakichaguliwa watauvuja Muungano, wanazungumza hadharani.Kwanini unagombea urais wa Tanzania wakati Tanzania huipendi, unapogombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maana yake unazungumzia nchi mbili huru.

"Unaona kabisa hao wagombea hata hawajui wanachokigombea, msiwachague watu wasiojua maana ya Muungano.Leo hapa kuna watu kutoka Pemba na Pemba nako kuna watu wa Bara, katika maisha ya dunia leo unapotaka kujenga uchumi lazima uangalie suala la kupata idadi ya watu na ndio maana ndani ya Afrika Mashariki tumeungana ili kutafuta soko la watu milioni 165 la Afrika Mashariki, nchi za SADC ziko 16 na idadi ya watu ni milioni 450.

"China idadi kubwa ya watu na ndio maana ni uchumi wake uko juu kutokana na idadi ya watu walionao kwani wako bilioni moja.India nako idadi ya watu ni kikubwa ya watu na huo ndio msingi wa uchumi.Mtu ambaye hajui uchumi unakoelekea maana yake hajui anachokiomba.Nimefafanua ili kujua umuhimu wa muungano, inazekana Tanzania mambo yetu yanafanikiwa kutokana na muungano tulionao,"amesema Dk.Magufuli.

Amesisitiza Tanzania kuna makabila 121, na nchi inaendeshwa kwa kwa pamoja, kwani kila kabila liko na huo ndio umoja wa taifa la Tanzania. Amesema kuna baadhi ya watu wanasema wakipata nchi wataigawa vipande, hivyo ameowamba wananchi kuwagopa kama ukoma.

"Nchi ya Afrika iligawiwa kwa vipande na walifanya hivyo Wakioloni mwaka 1884 hadi mwaka 1885, walitugawa.Huu si wakati wa kutugawa, hivyo tusikubali na kama taifa tumelisimamia vizuri,"amesema na kuongeza pia wamedumisha mapambano dhidi ya rushwa.

Amefafanua watu walikuwa wanaonewa na hata waliokuwa wakienda hospitali walikuwa wanaombwa rushwa na wanaoomba ni watu masikini, lakini ndani ya miaka mitano miaka mitano anataka kumaliza rushwa."Najua kuna wengine vichwa ngumu, mimi ni daktari wa kutumbua majipu, sijachoka hivyo nitaendelea kuyatumbua.Nataka watu wafurahie maisha, nataka watu wa Babati muishi kwa raha,

Kuhusu maendeleo ambayo yamefanyika katika Mkoa wa Manyara kwa miaka mitano iliyopita ni mengi na wananchi ni mashuhuda,huduma za kijamii zimeboreshwa na kwamba changamoto zilizobakia anakwenda kuzimaliza miaka mitano ijayo.

Pamoja na kuomba kura Dk.Magufuli aliamua kushughulikia changamoto ya wananchi waliomba kuunganishiwa umeme Babati na kuchelewa kupelekewa , ambapo ametoa maagizo kwa Waziri wa Nishati na Tanesco kumaliza changamoto hiyo ndani ya mwezi mmoja.

No comments: