DONALD TRUMP; MCHUMI, MFANYABIASHARA NA MWANASIASA ANAYETIKISA DUNIA
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
ANAFAHAMIKA kwa jina la Donald John Trump, Rais wa 45 wa Marekani akipokea kijiti kutoka kwa Barack Obama ambaye ni kiongozi wa kwanza mwenye asili ya kiafrika kuongoza taifa hilo, kabla ya kukabidhiwa ofisi hiyo Januari Mosi 2017 Trump alikuwa mtu maarufu na wengi walishangaa kuhusu Trump kuongoza taifa kubwa kama Marekani; alikuwa mfanyabiashara aliyemiliki majumba, hoteli za kifahari na majumba ya kamari.
Alizaliwa June 14, 1946 akiwa mtoto wa tano kati ya sita kutoka kwa Fred Trump mwenye asili ya Ujerumani na mama yake Mary Anne MacLeod kutoka Scotland, Trump alibahatika kutoka familia ya kitajiri na licha ya utajiri wa familia yake Trump alitegemea kufanya kazi ya ngazi ya chini kabisa katika kampuni za baba yake.
Alipofikisha miaka 13 akiwa shule ya awali alipelekwa katika shule ya msingi iliyofadhiliwa na jeshi na hiyo ni kutokana na utukutu alioufanya shuleni, na alifanikiwa kuhitimu elimu ya juu na kutunukiwa shahada ya uchumi katika chuo Pennsylvania mwaka 1968.
Katika safari yake ya mafanikio Trump alimwelezea baba yake Fred Trump, aliyefariki 1918 kwa homa ya mafua makali (Spanish Flue) kama mwongoza njia katika biashara zake na akafuata nyayo zake na alipofikisha miaka 27 tuu tayari alimiliki majumba ya biashara yapatayo kumi elfu yaliyokuwa chini ya kampuni ya Trump Management Corporation.
Katika maisha yake Trump amefanikiwa kumiliki na kuendesha shule ya mafunzo ya gofu katika maeneo mengi duniani ikiwemo Dubai, Scotland na Marekani na amewahi kutokea katika filamu za Home Alone na Lost in New York pamoja na mchezo wa World Wrestling Entertainment (WWE) maarufu kama mieleka, na amekuwa akitoa pesa nyingi za kuwasaidia wanajamii.
Trump hatumii kilevi wa kuvuta sigara, na hii ni kutokana na kuona namna kaka yake mkubwa Fred Trump Jr alivyoathirika na pombe hadi akapoteza uhai akiwa na miaka 43 pekee.
Hadi kufika 2020 kwa mujibu wa jarida la Forbes utajiri wa Trump uliripotiwa kufika dola za kimarekani 2.1 bilioni.
Trump ameoa mara mbili kabla ya kumuoa Melania Knaus mwaka 2005 na ana watoto watano na wajukuu wapatao kumi katika ndoa zake tatu.
Katika suala la siasa, Trump alijisajili uanachama katika chama cha Republican mwaka 1987, akahamia chama cha Independence mwaka 1999, mwaka 2001 akaenda chama cha Democratic na kurejea tena Republican 2009 na mwaka 2011 akahama chama hicho na kutangaza kutojiunga na chama kingine ila 2012 alirejea tena Republican, akagombea kiti cha urais na yupo madarakani kupitia chama hicho.
Novemba 3 mwaka huu Trump atapeperusha bendera ya Chama cha Republican kuwania awamu ya pili ya Urais wa nchi yake na anachuana vikali na Joe Biden kutoka Chama cha Democratic.
No comments: