DKT JOHN POMBE MAGUFULI JIANDAE KUAPISHWA...KURA YANGU MALI YAKO OKTOBA 28, SINA SHAKA UTASHINDA SANA




Na Said Mwishehe, Michuzi TV 


OKTOBA 28, mwaka huu Watanzania watafanya Uchaguzi Mkuu kuchagua Rais, wabunge pamoja na madiwani.


Ni uchaguzi unaokwenda kufanyika baada ya kampeni kwa vyama vya siasa na wagombea wao kunadi sera na Ilani zao kuhusu nini wanakwenda kukifanya kwa Watanzania.


Kwa mujibu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wagombea wa nafasi ya urais wako 15.


Ni wengi lakini ndio kukua kwa demokrasia ya siasa nchini katika mfumo huu wa vyama vingi ulioanza mwaka 1992 na Uchaguzi Mkuu wa kwanza kufanyika mwaka 1995. Ndio hivyo tu.


Tuachane na uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 na chaguzi nyingine zilizofuata za mwaka 2000, 2005, 2010 na mwaka 2015. Ngoja nijikite kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu 2020.


Uchaguzi utakaofanyika Oktoba 28,2020  itakuwa siku ya Jumatano na itakuwa ni ya mapumziko.


Tutapumzika ili kuwa na nafasi nzuri ya kwenda kupiga kura kuchagua viongozi ambao watatuongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.Ni uchaguzi muhimu kwetu Watanzania.


Ngoja nirejee hapo juu kidogo, nimeeleza kuwa wagombea wamefanya kampeni katika maeneo mbalimbali nchini, wamejinadi, wamejieleza, wametoa sera, wamefafanua Ilani zao, wametuomba kura, wameahidi yanayowezekana na yasiyowezekana, kimsingi tuseme wote tumewasikia.


Hata wagombea ambao wamezingumza mara moja au mbili na kisha kukaa kimya hadi kampeni zinafika ukingoni nao tumewasikia.Narudia tena wagombea wote tumewasiki.Tumewaelewa sana.


Kupitia mikutano ya kampeni tumepata nafasi ya kuwajua wagombea wote na hasa wa nafasi ya urais ambao ndio nimeamua kuwazungumzia zaidi.Angalau tunaweza kuzungumza chochote kuhusu wagombea hao. Wamejieleza sana aidha waliyotueleza hayana maana au yana maana.Shikilia tu wamejieleza na sasa ni zamu yetu kuamua.


Watanzania najua Oktoba 28,2020 tunakwenda kuamua, tukaamue vizuri,tukaamue nani tunakwenda nchi yetu aisimamie na kutuongooza vizuri.Kimsingi tunahitaji Rais wa Watanzania, tunahitaji Rais kwa ajili ya kutatua shida za Watanzania, tunahitaji Rais anayesimama na Watanzania wakati wote.Rais anayejua Watanzania wanakotaka kwenda kwa ajili ya nchi yao.


Ndio tunahitaji kuwa na Rais ambaye Watanzania tutamtuma na akakubali kutumwa kwa maslahi ya nchi yetu.Unashangaa nini ? Tunataka Rais ambaye atakuwa muongoza njia kwa maendeleo ya Watanzania.Huu sio uchaguzi wa kuchagua Rais atakayekuwa anaongoza nchi kwa kufuata maelekezo ya wasio watanzania.Hatutaki Rais wa kutumwa na mataifa makubwa kuhusu kutuongoza sisi Watanzania.


Kwa kuwa tumewasikia wagombea wote,ukweli sasa tunayo nafasi ya kuamua na naamini walio wengi wameshaamua nani awe Rais, wameamua kwasababu wamewasikia wakijieleza na wakitoa ahadi zao kupitia kampeni ambazo wamezifanya kwa zaidi ya siku 55 hivi, au chini kidogo au zaidi,kifupi wamejieleza kwa siku za kutosha.


Na si wapiga kura nikiwemo mimi tumeshaamua sehemu sahihi ya kupiga kura.Na kama nitabidilisha wazo kuhusu nani achukue kura yangu nitatumia siku ya leo na kesho na Jumatano kidogo kufika mwisho wa uamuzi wa yule ambaye naamini kura yangu itakuwa imekwenda kwa mtu sahihi.


Najua kura ni siri ya mpiga kura, huo ndio itaratibu, ndivyo tulivyozooea na ni utaratibu mzuri sana.Watanzania wenye sifa za kupiga kura watatumia utaratibu huo huo kuchagua kwa kupiga kura kwa siri.Karatasi ya mfano ya mpiga kura imetolewa na NEC,


Hivyo pamoja na kura kuwa siri lakini NEC imetusaidia kutuelimisha ili ninapochagua Rais niwe na hakika kura yangu iko salama.Hivyo tumewasikiliza wagombea na tumewasikia NEC na jinsi ya kupiga kura.Hili la tatu la kupiga kura linabaki kwetu .Watanzania twendeni tukaamue kuhusu hatma ya nchi yetu.Tuamue kupata Rais bora na sio bora Rais.


Tusipokuwa makini tunaweza kupata bora Rais badala ya Rais bora.Niwaombe Watanzania tuchague Rais bora badala ya bora Rais.Tunaweza kumpata Rais bora kama tutaamua kwa wingi wetu.


Binafsi namshukuru Mungu,kwanza kwa kunipa uhai na afya njema, na pili kwa kujipa ufahamu na uelewa pamoja na kupima na kuchuja kuhusu ninayoyaaona na kusikia.Nitatumia ufahamu wangu kupima hata yaliyosemwa na wanasiasa wakati wa kampeni.Wagombea naomba niwaambie binafsi nimeshawapima na ninaye ninayeamini anatufaa kwa wakati huu kuwa Rais.


Ni kweli kura ni siri lakini kura yangu inakwenda kwa Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli, ndio na huo utabaki kuwa ukweli kutoka ndani ya moyo wangu.Sina sababu ya kuficha, nimeshindwa kuvumilia,nimeshindwa kusubiri, kama nitakuwa nimekosa basi Tume ya Taifa ya Uchaguzi naomba mnisamehe,sio NEC tu hata vyombo vingine vinavyohusika na chaguzi naomba mnivumile.


Baada ya kuwasikiliza wagombea wote wa nafasi ya Rais,nimejiridhisha bila shaka yoyote mgombea huyo wa CCM ndio anastahili kutuongoza kwa miaka mitano.Ni Dk.John Magufuli, ametumia mikutano ya kampeni kueleza maono,mipango na mikakati ya nini yeye na Chama chake wanakwenda kufanya kwa miaka mitano.Amezungumzia yaliyomo katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2020-2025.


Mgombea huyo wa CCM ameeleweka sana, ameeleza nchi ilikotoka,iliko na inakokwenda.Sina shaka hata kidogo kwamba atashinda sana katika uchaguzi mkuu mwaka.Kama ambavyo nimetangaza rasmi kumpa kura yangu sitaki kuficha,naficha nini? Naogopa nini? 


Acha niwe muwazi.Najua hata unayesoma hapa umeshaamua nani awe Rais, sio lazima uwe kama mimi lakini naomba nikushawishi tu,ukifika katika chumba cha kupiga kura mpigie Dk.Magufuli.Kha! Aliyozungumza kuhusu Tanzania yamejaa matumaini makubwa kwa Watanzania,amezungumza atakavyosimamia rasilimali za nchi yetu.


Hapo mwanzoni nilivutiwa na sera za Hashim Rugwe ambaye anagombea urais kupitia Chama Chauma.Sera za kugawa ubwabwa zilinivutia sana, hata hivyo kadri siku zilivyokuwa zinasonga nikawa natafakari, nikabaini kuna maisha zaidi ya kula ubwabwa wa bure wa Rungwe.Kwa Tanzania yetu tunahitaji zaidi uboreshwaji wa miundombinu katika nyanja mbalimbali.


Tunahitaji kuwa na Tanzania ambayo itasimama imara kiuchumi,hivyo lazima tuwe na Rais atakeysimamia uchumi wetu.Hakuna mwingine zaidi ya Dk.Magufuli ,amethibitisha anaweza kusimamia uchumi wa nchi yetu, katika kipindi cha miaka mitano ametupeleka Uchumi wa kati kutoka nchi masikini.Unamuachaje Dk.Magufuli .


Tunataka kuwa na Rais ambaye atasimamia vema rasimali za nchi , na katika eneo hilo mgombea urais wa CCM ametuthibitishia anaweza.Amesimama imara katika kulinda rasilmali za nchi yetu.Amejenga hadi na ukuta kilinda Tanzanite yetu.Kule Mererani ukuta wa kilometa 25 umejengwa kuzunguka madini yetu.Ndio maana nasema kura yangu inakwenda kwa Dk.Magufuli.


Na kumpa kura yangu Dk.Magufuli haina maaana nawachukia wagombea wengine,haina maana hawafai kuongoza nchi hapana, wanaweza lakini kati ya wote hao Dk.Magufuli ana sifa zote za aina ya Rais ambaye Watanzania wanataka kuwa naye.


Nakumbuka wakati kampeni zikiwa katikati na zimepamba moto nilikuwa namfuatilia Mgombea wa Chadema Tundu Lissu, nikawa nasikiliza sera,ahadi na yale ambayo anataka kuyafanya kwa ajili ya Tanzania yetu, sio mbaya anaweza kutufaa lakini nimemuweka kando na sitampa kura yangu kwasababu hajafikia sifa alizonazo Dk.Magufuli


Hasa kipindi hiki ambacho Watanzania wanatakiwa kuwa wamoja, wanatakiwa kuendelea kudumisha mshikamano wao.Tundu Lissu anahubiri akiwa Rais ataongoza nchi kwa mfumo wa majimbo, kwangu hilo limeshindwa kuniingia akilini.Sitampa kura yangu.


Nampenda kaka Lissu lakini sio kiasi cha kusema nampa urais kwa kutumia kura nitakayopiga.Urais sio nafsi yake.Huna sababu ya kununa, kama wewe unaona anakufaa mpigie,kwani dhambi iko wapi ila nitakucheka kwa kweli 😂 😂 😂.


Kwa Bernad Membe anayegombea urais kwa kupitia ACT Wazalendo, sawa naweza kumpa Membe ,swali la msingi nampa kura kwa lipi? Huenda angefanya mikutano ya kampeni huenda angenishawishi, nakumbuka alifanya mkutano mmoja tu wa uzinduzi, akaka kimya, baadae alaenda Dubai kucheki afya.Hakuna wa kumlaumi ndio mipango yake.


Lakini nafahamu nadhani na wewe umesikia kuhusu Membe na yanayoendelea na Chama chake , wakubwa wenzake Zitto Kabwe na Maalim Seif Sharif Hamad wameshatangaza wao hawatamchagua Membe, usishangae na hao ndio wenye mgombea wao wa urais.Wametangaza watamuunga mgombea mwingine lakini sio Membe.


Hatari tupu lakini ndio siasa na wanasiasa wetu nchini.Swali la kujiuliza nampaje kura mgombea ambaye ndani ya Chama chake wanasema kwa Membe wao hapana.Wanamchagua yule wa Chama kile.


Kuna mambo ya msingi lazima ujiule Membe sawa ana sifa japo naye sio za kumfikia Dk.Magufuli lakini angalau.Sasa najiuliza nampaje kura wakati hata kwenye Chama chake haamini, mimi namuamini kwa lipi?Tena nimeona barua mtandaoni kuwa amejiondoa ACT Wazalendo.


Narudia tena kura yangu itakwenda kwa Dk.Magufuli,ni kiongozi  jasiri sana ,ni jasiri muongoza njia ya maendeleo.Ujue kwa Dk.Magufuli bahati kubwa yooooote ambayo amefanya tunaona, usipoona utaadithiwa, amefanya mengi ya kuonekana.Jamani tuache utani Dk.Magufuli ameijenga nchi ,kila kona maendeleo lundooo.


Vituo vya afya kila kona,hospitali za wilaya 68 mpya kajenga nchi nzima.Sijazungumzia elimu bure kwa shule za msingi na sekondari , watoto katika utawala wa Dk.Magufuli wanasoma bure,tunataka nini tena? Ninaposema nampa kura yangu naona aliyofanya.


 Nanda Kayla miundombinu ya barabara kuna mambo makubwa yamefanyika, leo hata kule Tandale na Buza jijini Dar kuna lami katik mitaa yetu.Taa za barabarani mwaaaaaa yani usiku kama mchana, hapo sijagusa barabara za juu pale Ubungo na Tazara.Kwenye usafiri wa anga, amefanyaa maajabu kutoka kadege kamoja kabovu hadi ndege 11 mpya.Huyo ndio Dk.Magufuli ambaye tayari ana uhakika kura yangu .Kura yangu Oktoba 28 ni kwa JPM tu.


Mzee wangu Profesa Ibrahim Lipumba najua anagombea urais kwa tiketi ya Chama cha Wananchi( CUF) .Prof .Lipumba sina shaka naye,sina ubaya naye,ni baba yangu,ni mzee wangu,sio utani ,mzee Lipumba tunafahamiana, ninashirikiana naye sana lakini kwenye urais kura yangu haiko kwake.


Ingawa akipata kura ya mwingine sina tatizo ,nitafurahi lakini kura yangu hapana, ana sifa zooote lakini katika urais moyo wangu unasita.Sijui kwanini? Na niliweka utamaduni wangu ninachokitilia shaka hata kama hakina tatizo naachana nacho.Uchaguzi mkuu mwaka huu mzee wangu utanisamehe.


Ila nikiangalia sana naona kama Prof.Lipumba naye atampigia kura Dk.Magufuli.Mzee wangu amua tu ,hakuna atakayejua.Kura ni siri,iwe siri yako.Mzee Lipumba nakutania tu lakini ukiamua sio mbaya.Maendeleo hayana Chama.Tumpe tu Dk.Magufuli aendeleze yale aliyoanza nayo.Tena nasubiri kwa hamu ile bima ya afya bure.Inatosha ila usisahau mwenzio kura yangu kwa JPM tumpe mitano tena.


Kwa ambaye nimemkwaza naomba anisamehe maana nimeamua kuweka wazi ninachokwenda kukifanya kwa ajili ya Dk.John Pombe Joseph Magufuli.Diamond nay ana mambo sanaa .Yeye anasema Magufuli Baba Lao.Ni kweli baba lao.


Nimalizie tu Ewe Mwenyezi Mungu ,muumba wa mbingu na vyote vilivyomo nikiwemo mimi na wewe atupe uzima na uhai ,ili Oktoba 28 nikamchague Dk.Magufuli.John Magufuli jiandae kwenda kuapishwa tu,kwa maoni yangu utashinda sana tena sana.Kweli tena.Ikiwa tofauti na ninavyofikiria nitashangaa.


Navyopendaga kupata marafiki wapya….ngoja nipachake na kanamba kangu 0713- 833822.



No comments: