AZAM FC YASAMBAZA UKWAJU SOKOINE.
Azam Fc imeendelea kumkimbiza mwizi kimyakimya licha ya kutotajwa sana katika mbio za ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara VP
L msimu huu 2020/2021.
Ikiwa ni muendelezo wa ligi kuu Tanzania VPL leo tarehe 20 mwezi October 2020 klabu ya Azam zawadi ya imegawa juisi ya ukwaju katika dimba la Sokoine jijini Mbeya kwa wageni wa ligi klabu ya Ihefu kutoka wilayani Mbarali Mkoani humo.
Alikuwa ni Ayoub Lyanga katika dakika ya 55 ya mchezo aliyeipatia Azam bao la kwanza akipokea krosi kutoka kwa kinara wa mabao ndani ya kikosi cha Azam Prince Dube huku kazi ya kugawa zawadi ya juisi ya ukwaju ikihitimishwa na Iddy Nado katika dakika ya 83 ya mchezo akipokea pasi ya bao kutoka kwa mwana Mfalme Prince Dube nakuzifanya dakika 90 za mchezo kumalizika kwa mabao 2-0 huku Azam wakiibuka washindi na Ihefu kuchachuka na juisi ya ukwaju kutoka Chamazi na kumkaribisha kocha Zuberi Katwila kwa kipigo katika klabu ya Ihefu.
Klabu ya Azam inabaki kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara VPL mara baada ya kucheza michezo 7 na kuvuna alama 21 huku wakiweka rekodi ya kushinda michezo yote Saba ya mwanzo wa ligi bila kupoteza mchezo wowote nao Ihefu wakishika nafasi 17 katika msimamo wa ligi wakiwa 3 walizovuna katika michezo 7 huku ndugu zao klabu ya Mbeya City wakiburuza mkia katika msimamo mara baada ya kufungwa na Mwadui Fc mabao 2-1 katika dimba la Chamazi Complex nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
No comments: