Chuo cha Kodi, TAFFA Waingia Makubaliano Kuimarisha Ujuzi wa Mawakala wa Forodha
Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA),Profesa Isaya Jairo na Rais wa Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Edward Urio wakibadilishana Mikataba mara baada ya kusaini jijini Dar es Salaam leo Machi 27, 2024.
Kulia ni Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA),Profesa Isaya Jairo na kushoto ni Raisi wa Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Edward Urio wakibadilishana Mikataba mara baada ya kusaini jijini Dar es Salaam leo Machi 27, 2024.
MKUU wa Chuo cha Kodi (ITA),Profesa Isaya Jairo amewataka wananchi pamoja na mawakala wa Forodha kutumia fursa ya kozi ya uwakala wa forodha Afrika Mashariki (EACFFPC) iliwaweze kufanya kazi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na sehemu yoyote Duniani.
Kauli hiyo imetolewa leo Machi 27, 2025 wakati wa hafla kusaini Makubaliano ya ushirikiano kati ya chuo cha kodi na Chama cha mawakala wa forodha Tanzani (TAFFA) wa usimamizi wa Kozi ya EACFFPC.
Amesema, wamelenga kuongeza ufanisi wa utendaji kwa mawakala wa forodha hivyo makubaliano hayo ni fursa muhimu kweo hivyo TAFFA haina budi kuwahamisha wanachama wao pamoja na jamii kunufaika na mafunzo ya uwakala wa forodha.
Amesema, wakala yeyote akiwa na cheti cha wakala wa Forodha cha Afrika Mashariki kutoka chuo chetu cha kodi anaweza kutumia cheti hicho kufanya kazi za uwakala wa forodha mahali popote ndani ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki na mahali popote duniani.
"Jumuiya ya Afrika Mashariki inahitaji Mawakala wa Forodha wenye weledi ambao watapunguza changamoto zinazojitokeza katika tasnia ya uwakala wa forodha na kukuza pato la Taifa." Amesema Profesa Jairo
Ameongeza kuwa, Chuo hicho kimekuwa mstari wa mbele katika ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika kwa kuwajengea uwezo watumishi wa mamlaka za mapato na hiyo ni kutokana na umahiri wake wa kuwa na wataalamu wengi waliobobea katika masuala ya forodha na kodi.
"Tunaowataalamu wengi waliobobea katika masuala haya hivyo tunaimani ushirikiano huu ambao tunauendeleza utaleta tija kwa wanachama wa TAFFA kwa kuwawezesha kufanya kazi zao kwa weledi na
kisasa zaidi huku wakihakikisha mapato yatokanayo na forodha yanaongezeka maradufu,"amesema Profesa Jairo.
Kwa upande wake, Rais wa Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Edward Urio amesema ushirikiano wanaoupata kutoka chuoni hapo ni mzuri kwani wao kama mawakala wa Forodha wako chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili waweze kutambulika na kuwa na leseni ya kufanya kazi za forodha.
"TRA ni kiungo muhimu kwao ili kuhakikisha wanakuwa na watendaji wenye weledi na kukidhi viwango vya kukusanya kodi pamoja na kutengeneza wafanyakazi bora watakaoweza kuingia kwenye soko la ushindani katika mipaka ya EAC na SADC ambapo kwa sasa dunia inakwenda kuungana katika nyanja mbalimbali.
Ushirikiano tuliosaini ni wa muda wa miaka mitano kukiwa na lengo la kuongeza ujuzi kwa mawakala wa Forodha na yatarejewa upya pale yatakapomalizika
No comments: