WILAYA YA TEMEKE KUJA NA MWAROBAINI WA KERO ZA WANANCHI
WILAYA ya Temeke imeandaa jukwaa la kutatua kero/changamoto za wananchi. Ambapo kwa siku 14, taasisi zote za serikali zitaweka kambi katika viwanja vya Mbagala Zakheem tarehe 14 hadi 20 Septemba na viwanja vya Mwembe Yanga kuanzia tarehe 22 hadi 28 Septemba.
Jukwaa hilo linajulikana kama "Temeke One Stop Jawabu". Ambalo ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuwataka wasaidizi wake na taasisi za umma kutatua kero/changamoto za wananchi. Hivyo katika eneo moja, taasisi zaidi ya 30 zitakutana, kusikiliza, kuhudumia na kutoa majawabu ya changamoto na kero hizo papo hapo.
Aidha miongoni mwa taasisi zilizothibitisha kushiriki katika jukwaa hilo ni NIDA, RITA, TANESCO, BRELA, TRA, LATRA,DAWASA, Taasisi za Kibenki, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Rufaa ya Temeke ambapo kutakua na upimaji wa afya na uchangiaji wa damu. Huku idadi ya wananchi wanaotarajiwa kuptiwa huduma inakadiriwa kuwa 200,000.
Sambamba na taasisi hizo, wanasheria Mawakili zaidi ya 20 kutoka chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS) 'chapter' ya Dar es Salaam watakuwepo kila siku kwa ajili ya kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi wote watakaobainika kuwa na changamoto zinazohitaji msaada huo.
'One Stop Jawabu' ni jukwaa ambalo linalenga kuzikutanisha taasisi zote za serikali na mashirika ya umma pamoja kwa ajili ya kutoa majibu ya changamoto na kero zinazowakabili wananchi.
No comments: