MAREKANI YAWATAKA WATANZANIA KUSHIRIKI UCHAGUZI, KUMCHAGUA KIONGOZI BORA

Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Dkt. Donald Wright akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi walipokutana kwa mazungumzo leo jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Dkt. Donald Wright amewataka Watanzania kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu ili kumchagua kiongozi bora atakayeweza kutekeleza malengo yao kimaendeleo.

Dkt. Wright amesema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi leo jijini Dar es Salaam ambapo wamejadili masuala ya ushirikiano wa maendeleo baina ya Tanzania na Marekani pamoja na kugusia harakati za kampeni za uchaguzi mkuu unaoendelea hapa Nchini.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.   Kabudi akimkabidhi Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Dkt. Donald Wright moja ya nakala ya kitabu kinachoelezea masuala ya uchaguzi mkuu nchini Tanzania
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.   Kabudi akimkabidhi zawadi ya picha Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Dkt. Donald Wright. Kulia mwa Waziri ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge.
*******************************
Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Dkt. Donald Wright amewataka Watanzania kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu ili kumchagua kiongozi bora atakayeweza kutekeleza malengo yao kimaendeleo.

Dkt. Wright amesema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi leo jijini Dar es Salaam ambapo wamejadili masuala ya ushirikiano wa maendeleo baina ya Tanzania na Marekani pamoja na kugusia harakati za kampeni za uchaguzi mkuu unaoendelea hapa Nchini.

Katika mazungumzo hayo Prof. Kabudi akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amemhakikishia Balozi wa Marekani Dkt. Wright kuwa Tanzania ni sehemu salama ya kuwekeza hususani katika sekta za utalii,kilimo,na biashara na kumhakikishia kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakuwa huru,haki na wa amani.

Prof. Kabudi ameongeza kuwa katika sekta ya utalii serikali ya awamu ya tano imedhibiti kwa kiasi kikubwa uwindaji haramu ikiwa ni pamoja na kupambana na ujangili jambo ambalo limeiwezesha serikali kuanzisha hifadhi za Taifa mpya nane ikiwa ni pamoja na kuimarisha hatua za usalama kwa watalii baada ya janga la corona kumalizika nchini.

Kwa upande wake Balozi wa Marekani hapa Nchini Dkt. Donald Wright amemhakikishia Waziri kabudi kuwa atahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji kuja nchini kuwekeza katika sekta za kilimo,biashara,huduma za afya na viwanda pamoja na kuhamasisha watalii kutoka marekani kuja nchini.

“Natumia pia fursa hii kuwasihi Watanzania kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu ili kumchagua kiongozi bora atakayeweza kutekeleza malengo yao kimaendeleo,” Amesema Dkt. Wright.

No comments: