WANAHABARI ARUSHA ,MANYARA NA DODOMA WAPEWA ELIMU KUHUSU UMUHIMU WA KILIMO CHA MBOGAMBOGA NA MATUNDA

Na Woinde Shizza Michuzi TV Arusha

Shirika la linalohusiana na utafiti mimea ya asili ya mbogamboga na matunda mkoani hapa (world Vegetable Center) limetoa mafunzo kwa wanahabari kutoka mikoa ya Manyara , Dodoma na Arusha ili kuweza kuelimisha jamii umuhimu wa kilimo hicho ambacho kinaleta tija katika sekta ya kilimo cha mbogamboga na matunda.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Dkt.Gabriel Rugalema ambapo alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kilimo cha mbogamboga kupitia kazi zao pamoja na umuhimu wa matumizi ya mbogamboga na matunda .

Alisema kuwa kilimo Cha mbogamboga ni muhimu kwa afya ya binadamu pia kilimo hichi ni muhimu kwa uchumi wetu kwani mkulima anapo lima na kuuza atakuwa amejiongezea kipato pia atakuwa ameweza kuingizia faida nchi ambayo itasaidia kukuza uchumi wa taifa letu.

Alitoa wito kwa serikali kuweka mkazo katika kilimo hicho ili watanzania waweze kutumia fursa ya kilimo hichi kujipatia kipato na kuondokana na umaskini kwani kilimo hicho kimeoneka kuwa chini katika nchi ya Tanzania huku wengi wao wakitumia kilimo hicho kwa matumizi ya nyumbani.

Alibainisha changamoto mbalimbali zinazokabili kilimo cha mbogamboga na matunda kuwa ni upatikanaji wa masoko na miundombinu kwa wakulima Jambo ambalo linakwamisha uendelevu wa kilimo hicho,uwepo wa wataalamu wachache hali inayosababisha uzalishaji mdogo wa mbogamboga hizo pamoja na elimu ndogo kwa wakulima juu ya kutumia fursa itokanayo na kilimo hicho.

Aidha Dkt.Rugalema aliiomba serikali kutanua sekta ya kilimo cha mbogamboga kwa kuweka mikakati itakayoendeleza kilimo hicho kwa kuweka mkazo na kutambua thamani yake

" Nchi yetu atuna wataalam wa ndani wa kutosha mwenye kilimo hichi Cha mbogamboga hivyo Naimani serikali ikiweka mkazo katika hili na kuanza kusomesha wataalam na kuwapeleka kwa wananchi wakawape elimu juu ya kilimo hichi tutapata wakulima wengi watakao Lima na tutaona manufaa ya kilimo hichi ikiwemo uchumi wetu kukua "alibainisha Rugalema

Kwa upande wake Meneja mauzo na masoko kutoka katika Kampuni ya uzalishaji mbegu ya East West Edilitruda Temba ameeleza kuwa kupitia kampuni yao wameweza kuwafikia asilimia 85 ya wakulima kwa kuwapatia elimu ya kilimo itakayo msaidia kulima kilimo chenye tija kitakacho kubalika sokoni na kumujngizia kipato.

Aidha ameongeza kuwa pamoja na lengo la kampuni hiyo la kuzaliza mbegu zenye ubora zitakazo muwezesha mkulima kupata soko pia wamsaidia mkulima mwenye kipato kidogo kuweza kulima kilimo chenye tiba kitakacho muwezesha mkulima kupata soko.

Vilevile ameongeza kuwa kutokana na changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakumba wakulima wa kilimo cha mbogamboga na matunda,kampuni hiyo imejikita kutoa elimu kwa wakulima juu ya umuhimu wa mbogamboga katika jamii kwa kuzingatia ubora wa mbegu.

Pamoja na hayo ameeleza kuwa kwa mwaka 2019 jumla ya wakulima 49126 walielimushwa kupitia kitengo cha wakulima ambapo pia wakulima wapatao 10558 waliweza kupatiwa elimu ya usambazaji wa mbegu kwa wakulima wadogowadogo.

Kwa upande wake mmoja wawashiriki wa mafunzo hayo Pamela Mollel alisema kuwa elimu aliyoipata itamsaidia kutambua umuhimu wa ulimaji Bora wa kutumia mbegu za asili ,pia atatambua faida za kilimo Cha mbogamboga ,pamoja na kutambua umuhimu wa ulaji wa mbogamboga katika jamii.



Mkurugenzi wa shirika linalohusiana na utafiti wa Mbogamboga na matunda (World Vegetables center) Dr.Gabriel Rugalema akiwaonesha waandishi wa habari namna wanavyolima na kufanyia utafiti mbegu za asili za mbogamboga wakati waandishi wa habari walipoanza mafunzo ya siku Saba ya kujua namna shirika Hilo linavyofanya kazi zake (Picha na Woinde Shizza ,Arusha)


Mkurugenzi wa shirika linalohusiana na utafiti wa mbogamboga na matunda (world Vegetables center) Dr.Gabriel Rugalema akiwaonyesha waandishi wa habari juzi namna wanavyolima na kufanyia utafiti mbegu za asili za mbogamboga wakati waandishi wa habari walipoanza mafunzo ya siku Saba ya kujua namna shirika Hilo linavyofanya kazi zake.(picha na Woinde Shizza ,Arusha).


Mtafiti msaidizi wa benki ya mbegu za asili kutoka shirika linalohusiana na utafiti wa mbogamboga na matunda (world Vegetables center) lililopo Tengeru Ndani ya halmashauri ya Meru Wilayani Arumeru mkoani Arusha Jeremiah Sigalla akionesha baadhi ya mbegu walizozihifadhi kwa kipindi Cha mda mrefu ,ambapo alisema benki hii ndio kubwa kuliko zote afrika inayoongozwa kwa kwa kuhifadhi mbegu nyingi (Picha na Woinde Shizza ,ARUSHA).


No comments: