MKENGE AOMBA CHUO CHA VETA BAGAMOYO ENDAPO ATASHINDA
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Muharami Mkenge, ametoa ombi kwa serikali la ujenzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi (VETA) ,ili kusaidia vijana wapate ujuzi wa masuala mbalimbali katika kujiinua kiuchumi.
Pia ameomba kipande cha barabara kutoka Daraja la Makofia mpaka Sunguvuni kuelekea Mashine ya Maji Ruvu chini, kiangaliwe ili magari yanayopeleka dawaa yapite kwa vipindi vyote.
Mkenge aliyasema hayo katika mkutano wake wa kwanza wa Kampeni kwenye uwanja wa Mgonela Kata ya Dunda jimboni hapa, ambapo alisema Chuo Cha Ufundi kitakuwa suruhisho kwa vijana kuajiliwa kwenye viwanda, kujiajili wenyewe sanjali na kuajili wenzao.
"Nilimkabidhi kilio cha ujenzi wa barabara ya Makofia mpaka Sunguvuni, ili kuyawezesha magari yanayopeleka dawa kwenye chanzo cha maji cha Ruvu chini yaende wakati wote, mwaka huu magari yalikwama kwa mvua, pia ifike mpaka Mlandizi," alisema Mkenge.
"Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli ni sikivu, kama tutakumbuka miaka mitano iliyopita mgombea weyu wa Urais Dkt. John Magufuli alipokuja kuomba kura kaka yangu Dkt. Shukuru Kawambwa alimuombaa kilometa tano za lami tayari zimeshajengwa," alisema Mkenge.
Mkenge aliongeza kwamba alipowasilisha maombi hayo kwa Mama Samia aliwaambia kwamba katika utekelezaji wa Ilani 2020/2025, barabara ya Makofia Mlandizi itajengwa kwa kiwango cha lami, na kulipwa fidia kwa wananchi wataopitiwa na mradi huo.
"Serikali ya CCM inapoahidi inatekeleza, mwaka 2015 kaka yangu Dkt. Shukuru Kawambwa alimuomba mgombea Urais mwaka huo Dkt. John Maguguli barabara ya lami kilometa 5, zimejengwa nami nikamuomba Mama Samia atuongezee kilometa tano nyingine," alisema Mkenge.
Kwa upande wake Mbunge aliyemaliza muda Dkt. Shukuru Kawambwa alisema ranaimani na Serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Magufuli, huku akisema kuwa Oktoba 28 akichaguliwa asimamie mchakato wa ujenzi wa Kituo cha afya barabara ya Bagamoyo Msata eneo la Fukayosi.
"Serikali ilitupatia pesa tukajenga Vituo vya afya Kerege na Matimbwa pia tukawa na mpango wa ujenzi mwingine Kata ya Fukayosi, nikuombe utakapochaguliwa simamia hilo, tunataka barabara zetu kubwa tatu zote ziwe na Vituo vya afya," alisema Dkt. Kawambwa.
Awali Mwenyekiti wa CCM wilayani hapa Alhaj Abdul Sharifu aliwataka wana-Bagamoyo kumchagua kwa kura za kishindo mgombea urais Dkt. John Magufuli, Muharami Mkenge, Apsa Kilingo na madiwani wote wanaotokea chama hicho.

No comments: