Wakulima wa parachichi wahamasishwa kutumia Mbolea ya asili

 Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya GUAVAY Ahad Katera,akizungumza kwa kifupi shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo wakati akihitimisha mafunzo ya siku moja kwa wasimamizi zaidi ya 70 wa mashamba ya parachichi zaidi ya ekari 900 mkoani Njombe,semina iliyofanyika Ukumbi wa JD Hotel mjini Njombe.
 Mtaalamu kutoka kampuni ya GUAVAY bwana Willium akitoa ufafaunizi juu ya Hakika maalumu kwa ajili ya kilimo cha parachcichi katika mafunzo kwa wasimamizi wa mashamba ya Parachichi iliyofanyika mjini Njombe.
Baadhi ya wasimamizi wa mashamba ya Parachichi wakiwa makini kusikiliza wakati semina ikiendelea kwa wasimamizi hao mjini Njombe.
 Wasimamizi wa mashamba ya Parachichi wakiwa kwenye picha ya pamja mara baada ya mafunzo ya siku moja juu ya matumizi ya Mbolea ya Hakika inayozalishwa na kampuni ya GUAVAY,mafunzo yamefanyika ukumbi wa JD Hotel mjini Njombe
  Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya GUAVAY Ahad Katera akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo mmoja wa wasimamizi wa mashamba ya parachichi aliyeshiriki katika mafunzo hayo.
Na Amiri Kilagalila, Njombe
ILI kukidhi ubora na kuingia katika masoko ya ushindani,wakulima wa zao Parachichi Nchini Tanzania wametakiwa kutumia mbolea za asili badala ya kutumia mbolea zenye kemikali hali inayosababisha kuanguka kwa zao hilo sokoni.

Wito huo umetolewa na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya GUAVAY Ahad Katera wazalishaji wa mbole mbali mbali ikiwemo Mbolea maalum katika zao la Parachichi Mbolea za HAKIKA,mara baada ya kufungua mafunzo rasmi kwa ajili ya wasimamizi wa mashamba ya Parachichi zaidi ya 70 wanaosimamia zaidi ya ekari 900 za mashamba ya Parachichi mkoani Njombe.

“Uwekezaji katika zao la parachichi unafanywa na watu tofauti tofauti,wakulima wa kati na wakubwa lakini ushauri na elimu wanaoupata katika kusimamia mashamba sio wa kitaalamu”Alisema Katera

Ameongeza kuwa “Kilimo cha parachcichi mkoani Njombe kinakuwa haraka sana lakini elimu na mafunzo ya ubora ni sehemu ambayo inatakiwa tuiwekee mkazo.Kmapuni ya Guavay inazalisha Mbolea ambazo ni asili ili kusudi mkulima anayelima Parachichi ambayo ni Organic kuww na utofauti wa bei na watu wengine”Aliongeza Katera

Wasimamizi wa mashamba ya Parachichi ambao ni wakulima mkoani Njombe akiwemo Chesco Mkolwe,Yohanes Njawike na Christina Myonga wamesema kilimo cha mazoea kimekuwa kikiwaingiza kwenye hasara kubwa na hii inatokana na kukosekana kwa wataalamu wa kutosha wa kilimo ambao wanaweza kuwapa elimu sahihi ya matumizi ya mbolea na dawa,hivyo kutokana na elimu iliyotolewa na wataalamu hao itasidia kuipga hatua kwenye kilimo.

“Sisi tunalima kilimo cha kuigana wenyewe kwa wenyewe kwa kuwa hatuna wataalamu wa kutuelekeza nah ii inatuathiri kwa kiasi kikubwa sana huku mashambani,kwa hiyo hapa leo tumejifunza mengi ambayo pia yanapunguza ghalama ya uzalishaji”alisema Chesco Mkolwe

Musa Makumba na Rebeca Mwepelwa ni wataalamu wa kilimo kutoka makampuni tofauti hapa nchini ambao wanatumia fursa hiyo kuwataka wakulima kuzingatia kanuni bora za kilimo na kulima kilimo hai.

“Sisi tunachotaka ni kufikia kwenye viwango vya kimataifa na kuweza kuhakikisha tunashirikiana kuhakikisha mtu anayetumia mbolea za kilimo hai atofautishwe na mtu anayetumia mbolea za Chumvi chumvi”alisema Musa Makumba

Kampuni ya GUAVAY ya jijini Dar Es Salaam ianayozalisha mbolea za Hakika ambazo ni asili imefika katika maeneo mbali mbali ya wakulima Nchini nchini huku mkoani Njombe ikifanya kazi na mawakala ili kuhakiksha inawafikia wakulima vijijini kwa bei naafu.

No comments: