WANAFUNZI WOTE WA SEKONDARI TUNDURU KUISHI BWENI


 Mgombea Ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma Happines Ngwando akiongea  na wanachama wa jumuiya ya umoja wa wanawake(UWT) katika mkutano wa baraza kuu la umoja huo lililofanyika mjini Tunduru ambapo amehaidi kama chama kitampa ridhaa ya kuwa Mbunge atahakikisha anashirikiana na wadau wengine wa maendeleo kujenga mabweni katika shule za sekondari kama mkakati wa kupunguza mimba kwa wanafunzi wa kike.
 Mgombea Ubunge wa jimbo la Tunduru Kusini Daimu Mpakate akitoa nasaha kwa wanachama wa jumuiya ya umoja wa wanawake UWT wilayani Tunduru.
 Mgombea Ubunge jimbo la Tunduru Kaskazini Hassan Kungu akiongea  na wanachama wa jumuiya ya umoja wa wanawake katika kikao cha kazi kwa viongozi wa jumuiya hiyo ikiwa  maandalizi ya kujipanga kuelekea kampeni za uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa wanawake wilaya ya Tunduru Zuhura Maftari akifungua mkutano wa baraza kuu la jumuiya  ya umoja wa wanawake(uwt)wilayani humo uliofanyika katika ukumbi wa uwt mjini Tunduru.
Picha na Mpiga Picha wetu

Na Mwandishi Wetu, Tunduru
MGOMBEA Ubunge Viti maalum Mkoa wa Ruvuma kupitia jumuiya ya Umoja wa  Wanawake wa chama cha Mapinduzi(UWT) Mkoa wa Ruvuma Happiness Ngwando amesema,iwapo chama cha Mapinduzi kitampa ridhaa ya kuwatumikia wanawake wa mkoa huo atahakikisha anajenga Hosteli kwenye Shule zote za sekondari kama hatua ya kutomesha mimba  kwa wanafunzi wa kike ambavyo vimekithiri katika wilaya ya Tunduru.

Ngwado ambaye  katika mchakato wa kura za maoni alishika nafasi ya  Tatu  akitanguliwa na Jackline Msongozi na Mariamu Nyoka, alisema hayo katika  kikao cha Baraza kuu la Jumuiya ya umoja wa wanawake wa Wilaya ya Tunduru kilichofanyika katika  viwanja vya baraza la Idd mjini hapa.

Katika kikoa hicho kilichohudhuriwa na wagombea wa majimbo ya Tunduru Kusini Daimu Mpakate,mgombea wa jimbo la Tunduru Kaskazini Hassan Kungu pamoja na baadhi ya waliokuwa wagombea wa ubunge viti maalum mkoa wa Ruvuma Sabina Lipukila na Habiba Mfaume.

Alisema, endapo atafanikiwa kupata ridhaa hiyo  kwa kushirikiana na marafiki na wadau mbalimbali wa maendeleo amejipanga kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu kunazia shule ya msingi hadi chuo kikuu kama njia ya kuwakomboa watoto wa kike wa Tunduru  dhidi ya vitendo hivyo ambavyo vimechangia wasichana wengi kuacha masomo.

Alisema mbali na mabweni kwa wanafunzi wa sekondari,mpango huo utakwenda  katika shule za msingi ili watoto wa kike waliopevuka(kuvunja ungo) nao waishi bweni.

Gwando amewaomba wanachama  na viongozi wa ccm kujiepusha na fitina,majungu na  kumaliza tofauti zao hasa wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu kwani umoja huo utakisaidia sana chama kufanya vizuri katika uchaguzi wa mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Ngwando amewashuruku viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya kwa kumuamini na kumchagua kuwa miongoni  mwa wagombea watatu waliochaguliwa  na mkutano  maalum wa uchaguzi wa uwt kuwa mkoa wa Ruvuma.

Aidha, amewataka wanawake wa umoja wa chama hicho kuhakikisha wanakuwa sehemu ya ushindi mkubwa wa wagombea wa chama cha mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka.

Alisema, wanawake ni jeshi kubwa lenye uwezo wa kuamua kila jambo hapa nchini,kwa hiyo ni lazima wahakikishe wanashirikiana na watu wengi kukipa ushindi wa kishindo chama hicho kuanzia ngazi ya udiwani,ubunge na Rais.

Alisema, kwa kutumia uzoefu alioupata katika mchakato wa kugombea nafasi ya viti maalum  kwa kushirikiana na viongozi wa chama, na wanachama wengine atahakikisha  kata zote na majimbo yote mawili ya Tunduru Kusini na Tunduru Kaskazini wagombea wa ccm wanapata ushindi mkubwa.

Katibu wa Uwt Mkoa wa Ruvuma Lukia Mkindu aliwaasa Viongozi wa jumuiya hiyo kuvunja makundi yaliyokuwepo wakati wa mchakato ndani ya chama na kuwa kitu kimoja hasa wakati huu wa kampeni na kukihakikishia ushindi Chama cha mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Alisema jumla ya wagombea 49 walijitokeza kuwania nafasi ya Ubunge viti maalumu mkoa wa Ruvuma na kwamba yeyote anayo nafasi ya kuteuliwa na chama kuwa Mbunge endapo Chama hicho kitapata ushindi wa kishindo katika mkoa wa Ruvuma.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wananwake (UWT) Mkoa wa Ruvuma Kuruthumu Mhagama alisema kuwa katika mchakato wa kuchagua wagombea haukuwa na upendeleo wala hakuna mgombea aliyeonewa wala kupendelewa.

Awali akitoa salamu, katibu wa chama Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Tunduru Kitte Mfilinge amewataka Viongozi wa Jumuiya hiyo kushirikisha waasisi wa Chama na jumuiya katika maeneo yao ili nao wapate nafasi za kuwa sehemu ya timu ya kampeni kwa kuwaombea kura wagombea  wa chama hicho.

Kitte alisema, huu ndiyo wakati muafaka kwa wana ccm kuunganisha nguvu na kwamba muda wa kutambiana umepita na kila mwanachama ashiriki katika kampeni za wagombea wa chama chao.

Amewaonya wanachama wanaotaka kwenda upinzani kutothubutu kufanya hivyo kwani sawa na kujipalia mkaa wa moto kwa sababu wasidhani heshima wanayopata ndani ya ccm wataipata wakihamia upinzani.

Baadhi ya wanachama wa chama hicho ambao walishiriki katika inyang’anyiro Sabina Lipukila na  Habiba Mfaule wamehaidi kuvunja makundi yaliyokuwepo na kuungana pamoja ili kufanikisha ushindi wa chama na wagombea waliopitishwa kugombea nafasi mbalimbali.

Sabina Lipukila amewataka wanachama wa CCM kuwa kitu kimoja ili kufanikisha ushindi wa chama katika uchaguzi mkuu ujao na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kukiangusha chama hicho.

“mchakato wa kura za maoni ndani ya chama umekamilika na tayari  kuna wanachama waliopitishwa kupeperusha bendera ya chama,kwa hiyo hakuna sababu ya kuendeleza makundi  yanayoweza kukiathiri chama chetu”alisema Lipukila.

No comments: