Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Longido Dkt.Jumaa Mhina akimkabidhi fomu ya uteuzi wa ugombea wa ubunge ya Tume ya Uchaguzi(NEC)Dkt. Steven Kiruswa kupitia tiketi ya CCM leo 24/8/2020
Mgombea ubunge jimboni la Longido Dkt.Steven Kiruswa kupitia tiketi ya CCM akisaini kitabu Cha kuthibitisha amepokea fomu ya uteuzi wa ugombea wa ubunge katika Jimbo hilo.leo tarehe 24/8/2020.Picha na Vero Ignatus.
Na.Vero Ignatus,Longido
Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la longido Dkt.Jumaa Mhina amewatoa hofu wananchi wa eneo hilo, na kusema kuwa uchaguzi utakuwa salama ,ukizingatia kuwa Jimbo hilo lipo mpakani ,kwani tayari wamevishirikisha vyombo vya dola kwamba mipaka ipo salama,katika kuhakikisha raia kutoka nje hawatashiriki katika uchaguzi.
Amesema hadi sasa tayari vyama vya siasa 6 ikiwemo CCM vimeshachukua fomu ya kwaajili ya nafasi ya ubunge, hivyo wamejipanga vizuri kuhakikisha kwamba kipindi chote cha uchaguzi kuwa amani imetamalaki pamoja na kutoa fursa sawa kwa vyama vyote vinavyogombea.
Amesema tayari wametengeneza ratiba ambapo vyama vyote vimeshapeleka,ambapo leo watakuwa na kikao cha vyama vyote kujadili ,watahakikisha ratiba inafuatwa.
Amesema kuwa endapo mgombea yeyote anatakwenda kinyume na taratibu za kawaida mbazo zimewekwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za tume ya uchaguzi ataitwa na kamati hiyo itatoa maamuzi
"Mara nyingi kunakuwa na kugombania maeneo ya kufanya Kampeni lakini yote haya tunao uzoefu wa kutosha maana siyo uchaguzi wa kwanza hivyo uchaguzi utakwenda salama salimini bila changamoto yeyote"alisema Dr.Mhina.
Akizungumza Mara baada ya kupokea fomu ya uteuzi wa ugombea wa ubunge katika Jimbo la Longido Dkt.Steven Kiruswa alisema kuwa atahakikisha kuwa Kampeni zake ataziendesha kwa ustaarabu,uadilifu,kwa kuzingatia na kutii kanuni taratibu na miongozo iliyowekwa na Serikali .
Amesisitiza na kuvisihi vyama vingine viendeshe Kampeni kwa Amani wasichafuane ,wasimamie Sera za vyama vyao,pamoja na malengo waaliyojiwekea kwa Yale ambayo watakuwa wameahidi kuwafanyia wananchi.
Amesema yeye atakuwa kielelezo w akufanya hayo yote kwa kushirikiana na chama chake Cha CCM pamoja kwa kufuata ilani ya chama hicho ya mwaka 2020-2025.
Kwa upande wake mwananchi kutoka Kata ya Cha kitumbeine amesema matarajio yao ni kwamba wao Kama wananchi wa Longido wanatarajia uchaguzi huo uende vizuri usiwe na vurugu kila mtu apate haki yake ili nchi iweze kuwa na Amani.
Amesema wanatamani wampate kiongozi ambaye hayakuwa na matabaka ya kubagua wale atakaowaongoza
Kwa upande wake Naijopi Olengilisho Kipaynoi Mkazi wa Kijiji Cha Ngarenaiboru amesema kuwa wao wanahitaji kiongozi anayeweza kuwaletea maendeleo hawataki mradi kiongozi
No comments: