MSIKITI MKUBWA WA KISASA WA GHOROFA MBILI KUJENGWA KISARAWE,WAISLAM WAMPA JUKUMU DC JOKATE MWEGELO


 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo(wa pili kushoto) akiwa na waumini wa Kiislamu wakielekea kukagua baadhi ya nguzo ambazo zimenza kujengwa katika Msikiti wa Wilaya hiyo.MSIKITI mkubwa wa kisasa wa ghorofa mbili ambao utakuwa Msikiti wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani unatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh.milioni 500 huku Mkuu wa wilaya hiyo Jokate Mwegelo akiahidi kusimamia ujenzi wa msikiti huo na utakamilika ndani ya mwaka mmoja.
 
 Waumini wa dini ya Kiislamu wilayani Kisarawe wakiwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Jokate Mwegelo wakiangalia baadhi ya nguzo za ujenzi wa msikiti mkubwa wa kisasa ambao unajengwa ndani ya wilaya hiyo.
 Waumini wa dini ya Kiislamu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani wakiomba dua maalum kwa ajili ya viongozi wa ngazi mbalimbali katika Serikali ya Awamu ya Tano, wakati walipokutana kuzungumzia ujenzi wa Msikiti wa Wilaya ya Kisarawe.Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo(hayuko pichani) ni miongoni mwa walishiriki kwenye dua hiyo.
 
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo(wa pili kushoto) akiwa na waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa kikao cha kujadili ujenzi wa msikiti mkubwa wa kisasa wa Wilaya hiyo ambapo Jokate amekubali ombi la kuwa mlezi wa kamati ya kufanikisha ujenzi huo.
 
Jokate Mwegelo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu wa Wilaya hiyo kuhusu ujenzi wa msikiti mkubwa wa kisasa baada ya kuombwa kuwa mlezi wa kamati ya ujenzi ambapo ameahidi kushirikiana nao ili kuufanikisha.
 
Waumini wa dini ya Kiislamu Wilaya ya Kisarawe wakiwa na Mkuu wa wilaya hiyo Jokate Mwegelo wakikaa kwenye viti baada ya kumalizika kwa dua maalumu ya kuwaombea viongozi wa kitaifa wakati wa kikao cha kuzungumzia ujenzi wa msikiti mkubwa wa kisasa wa wilaya hiyo.
 Waumini wa dini ya Kiislamu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakiwa wamekunja ngumi na kunyoosha mikono yao juu baada ya kumuomba Mkuu wa wilaya hiyo Jokate Mwegelo kuwa mlezi wao na kisha kukubali ombi hilo.
 
Baadhi ya nguzo ambazo zimeanza kujenga katika ujenzi wa msikiti wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.

 
Katibu wa Msikiti wa Wilaya ya Kisarawe Mohamed Bakari (kushoto)akisoma risala kuhusu ujenzi wa msikiti huo kwa mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo.
 
Msikiti Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani unavyoonekana kwa sasa ambapo tayari ujenzi wa kujenga msikiti mwingine mkubwa wa kisiasa umeanza na unatarajia kugharimu zaidi ya Sh.milioni 500.
 Waumini wa dini ya Kiislamu wilayani Kisarawe wakimsikiliza Mkuu wa wilaya hiyo Jokate Mwegelo(hayupo pichani) baada ya kukagua eneo ambalo utajengwa msikiti mkuu wa wilaya hiyo.
Katibu wa Msikiti wa Wilaya ya Kisarawe Mohamed Bakari akikabidhi risala ya ujenzi wa msikiti uo kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Jokate  Mwegelo.

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MSIKITI mkubwa wa kisasa wa ghorofa mbili ambao utakuwa Msikiti wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani unatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh.milioni 500 huku Mkuu wa wilaya hiyo Jokate Mwegelo akiahidi kusimamia ujenzi wa msikiti huo na utakamilika ndani ya mwaka mmoja.

Jokate ambaye ameombwa kuwa mlezi wa Msikiti huo wa Wilaya ya Kisarawe amewahakikisha waumini wa dini ya Kiislamu wilayani hapa kuwa anaamini hakuna kinachoshindikana na tayari ameanza kuzungumza na wadau wa ndani na nje ili kusaidia ujenzi huo na kwamba msikiti huo ukikamilika utakuwa umebeba taaswira ya wilaya hiyo ya Kisarawe.

Akizungumza na waumini wa dini hiyo wilayani hapa, Jokate Mwegelo amesema katika maisha yake hakuwa akifikiria kuna siku moja atapa heshima ya kuwa mlezi wa msikiti na kuombwa kushiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa msikiti lakini wananchi wa Kisarawe wamempa heshima hiyo ambapo amesisitiza hatawaangusha na atashirikiana nao bega kwa bega hadi msikiti ukamilike.

"Nimefurahi sana kwa heshima kubwa mliyonipa ya kuwa mlezi wa kamati yenu ya ujenzi yenye kuratibu shughuli za ujenzi wa msikiti wa Islamiya Kisarawe na niseme kwa dhati ya moyo wangu ahsante sana, nimeridhia kuwa mlezi na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu jinsi atakavyotuongoza naaamini sitowaangusha.Tutafanikisha ujenzi wa msikiti wetu huu wa Wilaya ya Kisarawe ambao utakuwa taaswira ya misikiti mingine ndani ya Wilaya yetu.

"Sisi sote tunafahamu msikiti ni taasisi inayojishughulisha na mambo mbalimbali ya kimaisha katika jamii ni pamoja na shughuli za maendeleo,kiuchumi na kiutamaduni na kwa mantiki hiyo kuwa na jengo la msikiti ni jambo muhimu katika kuratibu utekelezaji wa shughuli hizo,"amesema Jokate Mwegelo.

Amefafanua anaungana nao katika juhudi zote za ujenzi wa msikiti huo wa Kisarawe na atakuwa nao mguu kwa mguu, bega kwa bega hadi ujenzi ukamilike huku akisisitiza shughuli za uchumi na huduma ambazo zitakuwa zinatolewa na msikiti huo zitasaidia katika kupambana na umasikini, ujinga na maradhi , hivyo wananchi na taifa kwa ujumla litasonga mbele.

Amesema hata maandiko matakatifu ya Quraan yanaeleza Mwenyezi Mungu humpenda mja wake anayejituma katika kufanya kazi, hivyo akiwa mlezi wa kamati iliyoundwa kushughulikia ujenzi atajitajidi kadri Mungu atakavyomuwezesha kutoa mchango wake wa hali na mali kufanikisha ujenzi huo mkubwa na wa kihistoria, pia ameahidi atashirikiana na waumini wote, wadau wote na marafiki wote kuujenga msikiti wa Wilaya ya Kisarawe.

"Pamoja na kuzungumzia ujenzi wa msikiti huu, sote tunafahamu kwamba tuko kwenye kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28, 2020,hivyo nitoe rai kwenu Kisarawe, dini zote na wananchi wote kuzingatia amani na utulivu.Sitarajii uvunjifu wa amani ndani ya Wilaya ya Kisarawe.

"Na nimesema hivyo nikiamini viongozi wa dini ndio walezi wetu , ndio viongozi wetu wa dini ambao mko karibu na jamii, tuwasaidie vijana watulie, uchaguzi ufanyike kwa usalama na kisha tuendelee na majukumu yetu ya kuijenga Kisarawe.Mpaka tumefika hapa tayari Mungu ametufanyia wepesi tutaujenga msikiti huu huku tukiendelea kuwa watulivu,"amesema Jokate Mwegelo.

Amewaomba waumini wa dini hiyo na viongozi wa dini zote kwa ujumla kumuendelea kumuombea Rais Dk.John Magufuli ili aendelee kuwa mwenye afya njema na kuijenga nchi yetu kwa kuiletea maendeleo.

Awali akisoma risala kuhusu ujenzi wa msikiti huo, Katibu wa Msikiti wa Wilaya ya Kisarawe Mohamed Bakari amesema kwamba wazo la kuujenga msikiti huo ili uwe mkubwa wa kisasa lilianza mwaka 2000, na eneo lilipatikana mwaka 2006 na ilipofika mwaka 2007 wakapata ramani na ujenzi ukaanza mwaka 2018.

"Tulianza kuchanganishana fedha kupitia michango ya waumini wetu na katika kipindi cha miaka 10 tukafanikiwa kukusanya Sh.milioni 45 lakini ili msikiti huu ukamilike kama ramani ilivyo tunahitaji kupata zaidi ya Sh.milioni 500.

"Hivyo Mkuu wa Wilaya tunaomba nguvu yako ili tuungane pamoja kufanikisha dhamira hii ya waumini wa dini ya Kiislamu wa Kisarawe kuwa na msikiti mkubwa wa kisiasa,"amesema Sheikh Bakari. 

No comments: