Waziri Mkuu Majaliwa Aagiza ‘NBC Shambani’ Iwafikie Wakulima Wengi Nchini

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  (kulia) akijadili jambo na Waziri wa Fedha na Mipango Bw Phillip Mpango(kushoto), Naibu Waziri wa Kilimo Bw Hussein Bashe (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  NBC Bw Theobald Sabi (katikati)  wakati Waziri Mkuu alipotembelea banda la Benki hiyo lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Kilimo ya NaneNane  yanayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani  Simiyu. Wengine ni maofisa waandamizi wa Benki hiyo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  (wa tatu kushoto) akitazama moja ya bidhaa zinazozalishwa na mmoja wajasiliamali kampuni ya uzalishaji wa mafuta ya alizeti ya  Gilitu Enterprise ambao ni wateja wa benki ya NBC wakati Waziri Mkuu alipotembelea banda la Benki hiyo lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Kilimo ya NaneNane  yanayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani  Simiyu. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  NBC Bw Theobald Sabi (wa pili kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi  Bi. Zainab Telack na Meneja Bidhaa na Huduma za Kibenki kutoka Benki ya NBC Bw Jonathan Bitababaje (katikati).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa pili kushoto) akifurahia jambo na mmoja wa wajasiliamali ambae mteja wa Benki ya NBC Bi Melina Cheisa (kulia) wakati Waziri Mkuu alipotembelea banda la Benki hiyo lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Kilimo ya NaneNane  yanayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani  Simiyu. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack (katikati).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Katikati) akizungumza na Bw Hekela Sigalla (Kulia) kutoka kampuni ya utengenezaji wa mashine za samani (furniture) ya  Azienda Group ambae ni mteja wa benki ya NBC wakati Waziri Mkuu alipotembelea banda la Benki hiyo lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Kilimo ya NaneNane yanayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani  Simiyu. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  NBC Bw Theobald Sabi (wa pili kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi  Bi. Zainab Telack
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  (wa tatu kushoto) akitazama moja ya bidhaa zinazozalishwa na mmoja wajasiliamali kampuni ya uzalishaji wa pembejeo za kilimo ya Bajuta International ambao ni wateja wa benki ya NBC wakati Waziri Mkuu alipotembelea banda la Benki hiyo lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Kilimo ya NaneNane  yanayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani  Simiyu. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga  Bi. Zainab Telack.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  (kulia) akifurahia jambo na Waziri wa Fedha na Mipango Bw Phillip Mpango(katikati) , Waziri wa Kilimo Bw Japhet Asunga (wa tatu kushoto)Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (Kulia kwa Waziri Mkuu) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  NBC Bw Theobald Sabi (kushoto) wakati Waziri Mkuu alipotembelea banda la Benki hiyo lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Kilimo ya NaneNane  yanayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani  Simiyu.
 Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw Adam Malima (Katikati) akijadili jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  NBC Bw Theobald Sabi (kulia) pamoja na Meneja Uhusiano wa Benki hiyo ya Bw William Kallaghe wakati wakisubiri ujio wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye  banda la Benki hiyo lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Kilimo ya NaneNane  yanayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani  Simiyu.
NBC Hoyeee!!Waziri wa Fedha na Mipango Bw Phillip Mpango (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw Theobald Sabi (Kulia kwa Waziri) wakati Waziri huyo alipotembelea banda la Benki hiyo lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Kilimo ya NaneNane  yanayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani  Simiyu. 



 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza mawaziri wanaohusika na sekta za Kilimo na Fedha nchini kuhakikisha huduma mbalimbali za kifedha ambazo ni mahususi kwa ajili ya wakulima zinazotolewa na taasisi mbalimbali nchini ikiwemo huduma ya ‘NBC Shambani’ zinawafikia wadau wa kilimo na kuwaletea tija kulingana na makusudio ya kuanzishwa kwake.

Waziri Mkuu Majaliwa alitoa wito huo mwishoni mwa wiki alipotembelea banda la benki ya Taifa ya Biashara (NBC) lililopo kwenye Maonesho ya Kilimo NaneNane yanayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu.

Akiwa ameongazana na viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri wanaohusika na Kilimo, Uvuvi na Fedha, Waziri Mkuu Majaliwa alisema kwa kiasi kikubwa amevutiwa na huduma mbalimbali za kibenki ambazo ni mahususi kwa ajili ya wadau wa kilimo ikiwemo huduma mpya ya NBC Shambani ambazo zikisimamiwa vizuri na wadau wote ikiwemo serikali zitaleta tija kubwa kwa walengwa sambamba na kuongeza uzalishaji na ukuaji wa uchumi.

“Ufanisi wa huduma hizi mahususi kwa ajili ya wakulima utaleta muamko mkubwa kwao katika kufungua akaunti za kibenki, tofauti na huko nyuma ambapo walikuwa wanashindwa kufanya hivyo kwa kuwa huduma hizo zilikuwa haziwagusi moja kwa moja. Hivyo, pamoja na kuwapongeza benki ya NBC nawaomba Mawaziri msimamie hili kuhakikisha kweli huduma kama hii NBC Shambani na nyingine huko zinawafikia wakulima kulingana na malengo ya kuanzishwa kwake,’’ aliagiza.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo Bw Hussein Bashe alimuhakikishia Waziri Mkuu Majaliwa kuwa tayari Wizara hiyo ipo kwenye makubaliano na taasisi zote kubwa za kifedha nchini ikiwemo benki hiyo kuhakikisha wakulima wote wanakuwa na akaunti kwenye taasisi hizo ambazo hazitakuwa na makato kwa wakulima hivyo huduma hiyo ya NBC Shambani ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati huo muhimu.

“Lakini pia tulikubaliana AMCOS zote wanapopokea zile ‘AMCOS Fees’ waruhusiwe kutoa asilimia 50 ya hizo ada kwa ajili ya matumizi yao ila asilimia 50 ibaki kwenye akaunti zao kwa ajili ya kuendelea kuzalisha faida,’’ alifafanua.

Awali akimkaribisha Waziri Mkuu kwenye banda la Benki hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi alisema mbali na huduma hiyo ya NBC Shambani pia benki hiyo kwa kushrikiana na wadau wengine ikiwemo Jumuiya wa Jumuiya wa Wafanyabiashara wanawake na Vijana (TABWA) pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) iliendesha mafunzo maalumu ya kilimo na biashara yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu katika maonesho hayo.

“Ni jitihada kama hizi kwenye kilimo pamoja na kuwasaidia wajasiliamali kupitia vilabu vyetu vya kibenki ndio vimetuwezesha Benki ya NBC kuteuliwa ili kuwania tuzo za ubora za Afrika katika kuwahudumia wajasiliamali ambazo zinaakisi ufanisi wa huduma za kibenki na kifedha katika bara la Afrika.’’ Alisema.

Akifafanua kuhusu huduma ya NBC Shambani Mbele ya Waziri Mkuu Majaliwa. Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wakati, kutoka benki hiyo Bw Raymond Urassa alisema inalenga kuwasaidia wadau wa kilimo kutimiza malengo yao ya biashara ya kilimo ambapo inatoa fursa kwao kuwa na akaunti ya vikundi vya wakulima kama vile AMCOS na vikundi vingine pamoja na akaunti ya mkulima mmoja mmoja.

Alisema akaunti hiyo inawawezesha wakulima,wafugaji na wavuvi kufurahia huduma za benki hiyo bila kukatwa gharama zozote za uendeshaji kwani haina makato na zaidi mkulima atakapokuwa na akiba kiasi kinachozidi sh 100,000 kwenye akaunti yake atapatiwa faida kupitia riba.

Alisema akaunti hiyo inalenga wadau wote wanaojihusisha na biashara ya Kilimo wakiwemo wasambazaji wa pembejeo za kilimo, wakulima na wasafirishaji wa mazao ya kilimo.

No comments: