JOKATE AELEZA WALIVYOJIPANGA KUMALIZA CHANGAMOTO UHABA WA MADAWATI KWA WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jokate Mwegelo(wa pili kulia) akiwa na Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Isignia Ltd(Corol Paints)Vedastus Mzee(kushoto) na Meneja Masoko kwa kampuni hiyo Julieth Mdegela(kulia) pamoja na maofisa wa Idara ya elimu Misngi na Sekondari wakati akikabidhiwa msaada wa bidhaa za mbao na chuma kwa ajili ya kufanikisha utenegezaji wa madawati, viti na meza kwa ajili ya wanafunzi wa wilaya hiyo.
Jokate Mwegelo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani(wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msaada uliotolewa na Kampuni ya Isignia Ltd(Corol Paints) kwa ajili kusaidia utengenezaji wa madawati kwa ajili ya shule za msingi na sekondari ambapo wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo (kulia) akiwa na Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Isignia Ltd(Corol Paints) Vedastus Mzee wakishusha ndoo ya rangi kwenye gari.
Jokate Mwegelo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe( wa pilia kulia) akisisitiza jambo baada ya kupokea msaada kutoka Kampuni ya Isignia Ltd(Corol Paints).
Maofisa kutoka Kampuni ya Kampuni ya Isignia Ltd(Corol Paints) ya jijini Dar es Salaam wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jokate Mwegelo alipokuwa akielezea hatua zinazoendelea za utengenezaji wa madawati kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi pamoja na meza na viti kwa wanafunzi wa shule za sekondari.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Isignia Ltd(Corol Paints) ya jijini Dar es Salaam Julieth Mdegela akifafanua jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo.
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo(kulia) na Srinivasan Nelluvoy kutoka Kampuni ya Isignia Ltd(Corol Paints) ya jijini Dar es Salaam wakiendelea kushusha bidhaa zilizotelewa na kampuni hiyo kusaidia jitihada zinazoendelea za kutatua changamoto ya uhaba wa madawati. Picha na Said Mwishehe.

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WILAYA ya Kisarawe mkoani Pwani imesema inaendelea na mkakati wake wa kumaliza changamoto ya uhaba wa madawati kwa shule za msingi na pamoja na viti meza kwa shule za sekondari ikiwa ni jitihada za kuendelea kuboresha sekta ya elimu wilayani humo.
Hivyo kwa sasa Wilaya hiyo kupitia kiwanda chake kidogo imeanza kutengeneza madawati , viti na meza 2,699 na kazi hiyo inatarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jokate Mwegelo baada ya kupokea msaada wa gundi ya mbao, rangi ya mbao, rangi ya chuma, primer ya kuzuia kutu kwenye chuma pamoja na puti ya kujaza mashimo kwenye mbao  kutoka Kampuni ya Isignia Ltd (Coral Paints) ya jijini Dar es Salaam.

Jokate amesema msaada huo ambao umetelewa na kampuni hiyo umekuja wakati muafaka kwani ndio kipindi ambacho wanaendelea na utengenezaji wa viti, meza na madawati kama mkakati wa kumaliza changamoto ya uhaba uliopo shuleni.

"Nawashukuru kwa kuunga mkono juhudi za Wilaya ya Kisarawe katika kuboresha mindombonu ya elimu , kwani ninyi baada ya kuona tumeanzisha hizi harakati za kutokomeza upungufu wa madawati kwa shule na upungufu wa viti na meza kwenye shule za sekondari ambayo jumla yake ni  2699.
"Mmevutiwa na kuja kutushika mkono Kisarawe katika jitihada hizi ambazo tunazifanya kwa kiwango cha ubora na viwango.Mmekuja wakati sahihi kwasababu ndio kipindi ambacho matokeo ya kidato cha sita yametoka na shule yetu ya Mwanarumango katika matokeo yake ya kidato cha sita mwaka huu hakuna aliyepa daraja sifuri.

"Hata Sekondari ya Minaki imefanya vizuri licha ya kuwa na wanafunzi waliohitimu 323 na kutokana na usimamizi mzuri kwa wanafunzi hao zero iko moja tu , waliopata daraja la nne wako wa wawili na waliobakia wote ni daraja la kwanza, la pili na tatu,"amesema Jokate na kusisitiza mafanikio hayo yanatokana na mipango madhubuti na usimamizi mzuri ambao wameuweka kwenye sekta ya elimu.

Amesisitiza kwa hiyo wataendelea kuboresha elimu katika Wilaya yao ya Kisarawe  ikiwa ni kuunga mkono juhudi na maono ya Rais Dk.John Magufuli ambaye yeye kupitia serikali ya Awamu ya Tano ameweke sera ya elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari.
"Elimu ya misingi hadi sekondari ni elimu bila malipo kwa maana ya kwamba ada inalipwa na Serikali na hilo limetimizwa, ni jambo ambalo limetoa hamasa kubwa kwa watoto na vijana kutokuwa na vizingiti vya kupata elimu.

"Utoaji elimu bila malipo umesaidia kuondoa mawazo hata kwa baadhi ya wazazi na walezi nao sasa hawana visingizio tena na tunachowaamba ni kuhakikisha wanatusaidia katika malezi bora, mavazi, malazi na chakula lakini kwenye ada Serikali imebeba jukumu hilo,"amesema Jokate.
Ameongeza inafahamika Taifa lenye watoto na vijana wasiokuwa na elimu ni mfu na haliwezi kusonga mbele."Na sasa  tuko uchumi wa kati na sote tunafurahia lakini kuendeleza hiyo spidi hakuna budi kusomesha vijana na watoto kupata elimu."

Amesisitiza jukumu ambao wanalo viongozi wa ngazi mbalimbali ni kusaidia kutafsiri maono ya Rais kwa ajili ya kuleta maendeleo huku akitumia nafasi hiyo kuelezea hatua kwa hatua namna ambavyo wilaya ya Kisarawe imesimama imara kuboresha miundombinu ya elimu na kuhakikisha kampeni ya tokomeza Zero inaendelea kuzaa matunda.

Kwa upande wa Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Isignia Ltd Vedastus Mzee amesema wameamua kutoa msaada huo ambao sio mara ya kwanza kutokana na jitihada ambazo wamekuwa wakiziona katika sekta ya elimu wilayani humo.

Na kwamba kampuni yao itaendelea kusaidia kadri watakavyoweza ikiwa ni sehemu pia ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli ambayo imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji."Tumetoa msaada wa bidhaa tulizonazo kwa upande wa mbao na chuma, hasa kwa kutambua vitakwenda kusaidia katika kipindi hiki cha kutengeneza madawati."

No comments: