WANACCM PWANI WATAKIWA KUUNGANA KUSAKA USHINDI WA MAFIGA MATATU

Mwamvua Mwinyi, Pwani
MJUMBE wa halmashauri kuu ya CCM (MNEC) Mkoani Pwani ,Hajji Jumaa amewasihi wanaCCM kuwaunga mkono na kwenda nao pamoja wabunge na madiwani wateule, waliopitishwa na vikao vya juu vya chama ili kupata ushindi wa kishindo na kutimiza mafiga matatu ifikapo uchaguzi mkuu oktoba mwaka huu.

Aidha ameeleza,Kati ya kata 141 za Mkoa wa Pwani washindi waliopita kura za maoni wamerudi isipokuwa kata moja ya Vikindu, huku nafasi ya Ubunge ni jimbo moja la Kibaha Vijijini, ndio mgombea wake alieshinda akuweza kupitishwa, ambapo ni kama mikoa mengine ilivyofanyika na sio kuona ajabu mkoa huo.

Akielezea, kuelekea kipindi cha kampeni na namna mkoa ulivyojipanga katika uchaguzi mkuu,alisema hatua ya vikao vya mchujo mkoa,ilikuwa ngumu lakini walimtanguliza Mungu mbele na haki ya kila mtu iliheshimiwa sanjali na kuweka maslahi ya Chama mbele.

Jumaa aliwaasa, wanaCCM na Wanapwani kuhakikisha wanakwenda kuitafuta kura ya Rais dkt.John Magufuli kokote iliko na za Wabunge na Madiwani wa mkoa wa Pwani ili kuibuka kidedea.

"Tuache umimi ,chama sio mtu ,tujali na kuangalia maslahi ya chama chetu na kuondoa chuki na makundi kuanzia sasa ,na badala yake tuungane na kuwa kitu kimoja. " Alisisitiza Jumaa.

Hata hivyo, aliwapongeza wagombea wote waliopita katika vikao vya mchujo, na vile alivyoviongoza akiwa Mwenyekiti wa muda wa CCM Mkoa Pwani,na kusema Chama Kwanza, Ushindi Kwanza .

"Niwaombe wanachama wa CCM na Kibaha Vijijini kuungana na Chama Cha Mapinduzi maana Chama sio Mtu, Chama ni taasisi, tuhakikishe Mgombea wetu anashinda kwakuwa anasifa za kuwa Mbunge wa Kibaha Vijijini kupitia Chama Chetu."

Jumaa alifafanua,wagombea wote ni wazuri kwakuwa walipita kwenye vikao na alipata bahati ya kuwa Mwenyekiti wa vikao vya awali kwa ajili ya mapendekezo kwa vikao vya juu.

Anabainisha, wagombea wote wanajua agenda za Mkoa wetu, wagombea ambao wanajua Pwani wapi inataka kwenda watu wa Pwani wanataka nini,niwaombe kwa umoja tuwaunge mkono, tuwasadie, tuwashauri na tuendelee kuwaelekeza pale panapotakiwa kufanya hivyo.

No comments: