GCLA:Madereva kujikinga na madhara ya kemikali wakati usafirishaji wa kemikali hizo


 Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv .

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imesema kuwa madereva wanatakiwa kutumia njia ya bora   ya kukabiliana au kujikinga na madhara ya kemikali  kwa lengo la kulinda afya na Mazingira pindi wanaposafirisha bidhaa hiyo.

Hayo ameyasema Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali Sebanito Mtega wakati akifunga mafunzo ya madereva wanaosafirisha Kemikali ndani ya Nchi na Nje ya nchi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mtega amesema kuna ajali ilitokea Beirut Lebanon ilihusisha tan 2,750 za kemikali ya Amonium Nitrate na  kuua watu zaidi 135 na kujeruhi zaidi ya watu 5,000 huku kuacha watu zaidi 300,000 bila makazi .

Hata hivyo amesema kuwa ajali ya Lori la mafuta  lililowaka na Msamvu mkoani Morogoro Agasti 9 na kusababisha watu 70 kupoteza maisha na 59 walijeruhiwa pamoja na mali kuteketea.

Mtega amesema kuwa katika matukio hayo madereva ni watu wa kwanza katika kukabiliana na majanga hayo yasitokee kutokana na madhara yake kuwa makubwa kwa afya na mazingira.

Mtega amesema kuwa GCLA imepewa jukumu  na serikali kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wanaojihusisha na shughuli za Kemikali ikiwamo usafirishaji salama wa kemikali hizo.

Amesema mafunzo hayo yamefanya madereva kuwa na weledi wa usafirishaji salama wa kemikali na hivyo kuimarisha jitihada za utekelezaji wa sheria namba 3  ya mwaka 2003 ya  udhibiti na usimamizi wa Kemikali za Viwandani na majumbani.

Aidha amesema kuwa madereva wanapokuwa wanasafirisha Kemikali kuzingatia usalama Kemikali hizo wakati wanapoanza safari hadi wanashusha mzigo huo.

Mmoja madereva Abdulrazak Omary amesema kuwa mafunzo waliyoyapata ni kwenda kutekeleza namna ya kuchukua tahadhari za kiusalama pamoja kutoa tahadhari kwa wananchi walikuwa kandokando ya barabara kuacha kukimbilia pale inapotokea ajali.

Dereva wa Burundi Ndayishimiye Haruna  amesema kuwa kuna vitu alikuwa hajui lakini sasa amepata elimu na kuishukuru GCLA kwa kuwa na utaratibu wa mafunzo.
 Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali Sebanito Mtega akizungumza wakati akifunga mafunzo kwa madereva  kuhusiana kukabiliana au kujikinga na madhara ya Kemikali yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Idara ya Usimamizi wa Kemikali  wa (GCLA) Daniel Ndiyo  akitoa maelezo kuhusiana na mafunzo ya kuwajengea uwezo madereva jinsi kuchukua tahadhari ya madhara ya Kemikali ,jijini Dar es Salaam.
 Dereva Abdulrazak Omary akizungumza kuhusiana na umuhimu wa mafunzo kuhusiana na kemikali,jijini Dar es Salaam.
 Dereva wa Burundi Ndayishimiye Haruna akizungumza namna ya kuwa balozi wa kutoa elimu kuhusiana madhara ya Kemikali,jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali Sebanito Mtega akimkabidhi cheti  cha mafunzo dereva mara baada ya kufungwa mafunzo hayo,jijini Dar es Salaam.
Madereva wakiwa katika ya mafunzo ya madhara ya Kemikali wakati wakisafirisha yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 

No comments: