CHRISTIAN BELLA, OMMY DIMPOZ NDANI YA BSS 2020

  Jaji wa Mashindano  kusaka kipaji, Johakim Kimario, 'Master J' akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. kulia ni muandaaji wa shindano la BSS, Ritha Paulsen, 'Madam Ritha'.
Mwanamziki, Christian Bella  akizungumza wakati wa kutangazwa kuwa majaji wa BSS mwaka huu. Kulia ni muandaaji wa shindano la BSS, Ritha Paulsen, 'Madam Ritha'.

 Na Khadija seif, Michuzi tv
SHINDANO la kusaka vipaji, Bongo Star Search, (BSS) msimu mpya wa 11 kuanza Septemba 19, 2020 mkoani Mbeya, wametambulisha majaji  wapya wawili kwenye shindano hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa kutangaza majaji, muandaaji wa shindano hilo, Ritha Paulsen, 'Madam Ritha' amesema mwaka huu wamefanya mabadiliko katika safu  ya majaji.

"Napenda kuwataarifu kuwa msimu wa 11 majaji watakuwa ni Chief jaji Madam Ritha, Johakim Kimario, 'Master J', Christian Bella, Omary Nyemo,'Ommy Dimpoz', na mshehereshaji wa kipindi atakuwa Idris Sultan".

Pia usahili utaanza kwenye mkoa wa Mbeya Septemba 19, Dhamira Hall, Point Zone Resort,  Arusha Septemba 26 na Mwanza Octoba 3 Isa milo hotel, na 10 itakuwa Mkoani Dodoma, Royal na Dar es Salaam itakuwa ni Octoba 17 na 18 itafanyika Makumbusho ya Taifa".

No comments: