ALIYETIA NIA JIMBO LA ARUMERU MAGHARIBI AHAMASISHA UMOJA KWA WANA CCM KUFANIKISHA USHINDI KWA ALIYEPITISHWA NA CHAMA KUPEPERUSHA BENDERA

Picha ikionyesha mtia Nia wa Jimbo la Hai ambaye Kura zake hazikutosha Martin Munisi kulia akiwa na mtia Nia wa Jimbo la Arumeru magharibi Ezekiel Mollel wakibadilisha mawazo ambapo wagombea wote Hawa walisema japo hawajapita katika kimyangany'iro cha kura za maoni CCM wamejipanga kuwapa ushirikiano wa kutosha wagombea waliopitishwa na Chama chao kupeperusha bendera (Picha na Woinde Shizza, ARUSHA)
 

Na Woinde Shizza , michuzi Tv ARUSHA

KADA wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Ezekiel Mollel ambaye ni moja ya waliotia nia katika Jimbo la Arumeru Magharibi amejitosa kumuunga mkono mgombea mteule wa Chama hicho Noar Lembriss Mollel huku akieleza hiyo ni operesheni kabambe ya kulikomboa jimbo hilo ambalo liko katika mikono ya wapinzani.

Akizungumza  na vyombo vya habari leo Ezekiel Mollel ambaye alikuwa ni miongoni mwa waliokuwa watiania 61 wa jimbo hilo amekipongeza Chama chake kwa kumteua Noar Lembris na kwamba uamuzi huo unapaswa kuzingatiwa na wana CCM kwani zamu yake bado na kuwataka kumuunga mkono mgombea huyo.

Ezekiel amekuwa kada wa kwanza kujitokeza hadharani kumuunga mkono mteuli huyo Lembris Noar ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha kupitia Chama cha CHADEMA  kabla hajahamia CCM, akidai kuwa nia yake ya dhati ni kuona jimbo la Arumeru Masharibi linatoka upinzani .

"Nipo tayari kusubiri wakati mwingine wa kuwania nafasi ya Ubunge ila kwa sasa itoshe kueleza kwamba nguvu yetu kubwa ni kukomboa jimbo la Arumeru Magharibi.Wana CCM tuache makundi na kuungana, tuwe wamoja ili kukiwezesha Chama kupita kwa kishindo.

"Nimesikia kuna watu wameanza makundi kutokana na matokeo yaliyotokea nachotaka kusema kiongozi analetwa na Mungu kama nafasi yako imefika utapita tu, sasa basi kinachotakiwa sisi kama Wana CCM tumuunge mkono kiongozi yeyote yule aliyependekezwa na Chama chetu kiweze kupata ushindi ,tupate ushindi kwa mafiga matatu Rais ,Ubunge na madiwani,"amebainisha Ezekiel

Jimbo hilo kwa sasa linaongozwa na Chadema chini ya mbunge aliyemaliza muda wake Gibson Ole Meseiyeki ambaye amepata tena uteuzi wa kupeperusha bendera ya Chadema .

No comments: