WATANZANIA WATAKIWA KUEPUKA HABARI ZA UZUSHI
Watanzania wametakiwa kulisemea mambo mazuri Taifa lao ili kuwa na kidiplomasia nzuri na Mataifa mengine hususani wakati huu ambapo Taifa linaomboleza kifo Hayati Benjamini William Mkapa na kuachana na habari za upotoshaji zinazoenezwa katika mitandao ya kijamii hasa baada ya ujumbe wa Kenya uliokuwa ushiriki katika maziko ya kitaifa Jijini Dar Es Salaam kushindwa kufika kama ilivyokuwa imepangwa
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Damas Ndumbaro ameyasema hayo jijini Dar es Salaam kufuatia kuenea taarifa za uzuishi katika mitandao ya kijamii hususani baada ya ujumbe uliokuwa uiwakilishe Kenya katika maziko ya kitaifa yaliyofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kushindwa kufika na ndege iliyokuwa imewabeba wajumbe hao kurejea Kenya.
Dr.Ndumbaro ameongeza kuwa kuandika au kuchapisha taarifa za uzushi na zisizo na uthibitisho ni kinyume cha sheria za mitandao yam waka 2015 na adhabu yake ni pamoja na kifungo gerezani.
No comments: