RAIS DKT. MAGUFULI AKIPITA KWENYE DARAJA LA MKAPA RUFIJI MKOANI PWANI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipita na kukagua Daraja la Mkapa linalopita katika Mto Rufiji mkoani Pwani wakati akitokea Masasi Mtwara kwenye msiba wa Marehemu Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa leo tarehe 30 Julai 2020. Daraja hilo linalounganisha Pwani na Mikoa ya Lindi na Mtwara lilijengwa na Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Marehemu Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa.
No comments: