UJENZI MRADI WA MAJI MKURANGA WAFIKIA ASILIMIA 80


Na Zainab Nyamka, Michuzi TV.
 
UJENZI wa Mradi wa Maji wa Mkuranga umefikia asilimia asilimia 80 unaendelea kutekelezwa kwa kasi ili kukamilika kwa wakati na wananchi kuanza kupata huduma ya maji safi.

Mradi huo unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam DAWASA unahusisha ujenzi wa tanki la lita milioni 1.5 na ulazaji wa mabomba ya usambazaji.

Ujenzi wa mradi huo ni muendelezo wa kisima walichochimba eneo la kurungu mwaka 2015 ukijengwa kwa thamani ya bilioni 5.5 kupitia mapato ya ndani utajumuisha ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita milioni 1.5 tenki la kupokea na kusambaza maji hadi kwenye tanki sambamba na ulazaji mambomba urefu wa kilomita (63) hadi Vikindu.


Maeneo yatakayonufaika kuwa ni pamoja na Mkuranga A,B,Kiguza,Bigwa,sambamba na Mkwalia Kitumbo,Njia Nne, Hoyoyo.

Mradi huo utakapomalizika utahudumia wakazi 25,500 sawa nan asilimia 83 ambapo kwa sasa jumla ya wakazi 4500 sawa na asilimia 17.6 ndiyo wanaopata maji safi na salama.
 

No comments: