WAZAWA WAASWA KUONDOA HOFU YA KUCHANGIA MAENDELEO YA WILAYA YA IRAMBA MKOANI SINGIDA

SERIKALI wilaya ya Iramba mkoani Singida, imetoa wito kwa wazawa wa ndani na nje wa wilaya hiyo, waondoe hofu kuchangia maendeleo ya wilaya yao kwa madai itahusishwa na vitendo vya rushwa na badala yake waongeze kasi zaidi kuchangia kwa hali na mali ili wilaya iendelee kupaa kimaendeleo.

Wito huo umetolewa juzi na mkuu wa wilaya hiyo, Emmanuel Luhahula, wakati akitoa shukrani na pongezi kwa wizara ya maji kutoa msaada wa vifaa vya kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona. Msaada huo umetolewa kwa shule ya sekondari ya Tumaini tarafa ya Kinampanda.

Amesema maendeleo ya kweli ya wilaya Iramba, yataletwa na wazawa, serikali na wadau wengine watasaidia juhudi hizo.

"Hii hofu potofu ya kila msaada kuhusishwa na rushwa ikiachwa iote mizizi, itaathiri kwa kiasi kikubwa maendeleo ya wilaya ya iramba. Huu msaada wa leo umetoka wizara ya maji kwa asilimia mia moja",amesema na kuongeza;

"Serikali imenileta wilaya ya Iramba kutekeleza majukumu ya serikali na si vinginevyo. Sijaletwa Iramba kufanya kazi za kisiasa. kwenye siasa mimi sipo".

Kwa upande wake katibu mkuu wizara ya maji Profesa Kitila Mkumbo, amesema serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kupeleka maji safi na salama kwenye shule na vituo vya afya.


Amesema shule, vyuo vikubwa na maji ya kutosha wanafunzi wataendelea na masomo yao kwa utulivu mkubwa. Pia kwenye vituo vya afya, wanawake watajifungua kwa amani.

Naye mkurugenzi wa huduma za ubora wa maji wizara ya maji, Philipo Chandy, amesema vitakasa mikono vilivyotengenezwa na wizara hiyo, vina ubora unaokidhi mahitaji.

"Quick Land Sanitizer ambayo ni miongoni mwa msaada tuliomleta, ni bora kabisa. Kila mwanafunzi atapata moja ambayo ataitumia kwa mwezi mzima. Msaada huu hautaishia kwa wanafunzi tu, walimu na wafanyakazi wengi watapatiwa",alisema.

Mwanafunzi wa kidato cha sita, Catherine Majaliwa, amemshukuru Rais DK.Magufuli kwa uamuzi wake kuruhusu warejee shuleni kujiandaa na mtihani. 

"Serikali ya Dk. Magufuli kupitaia wizara ya maji imeichagua shule yetu ya Tumaini kupata msaada huu.Tunashukuru sana. Tutahakikisha hatumwangushi Rais wetu anayejali wanafunzi na Watanzania wengine. Tutafanya 'wonders' kwenye matokeo mtihani wa kidato cha sita mwaka huu. 

Wakati huo huo,Profesa Kitila ametumia fursa hiyo kuwaangiza wanafunzi hao waendelea kuchukua tahadhari kwa kujikinga na kudhibiti na kusambaa virusi vya Corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu. 

Aidha,amesema kuwa wizara ya maji imejipanga vizuri kwa ajili ya kuhakikisha shule,vyuo na vituo vya afya nchi nzima zinapata maji safi na salama.
 Katibu mkuu wizara ya maji,Profesa Kitila Mkumbo,akizindua chombo cha kunawia mikono kilichotolewa na wizara maji kwa shule ya sekondari Tumaini wilaya Ikungi.Lengo ni kujikinga na corona.Wa kwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Iramba,Emmanuel Luhahula.
 Katibu mkuu wizara ya maji,Profesa Kitila Mkumbo,akitoa nasaha zake kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vilivyuotolewa na wizara maji kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa.Vifaa hivyo vimetolewa msaada kwa shule ya sekondari Tumaini Kinapanda wilaya ya Iramba.
  Katibu wizara ya maji Profesa Kitila Mkumbo pamoja na wanafunzi shule sekondari Tumaini wilaya ya Iramba,wakifurahia msaada uliotolewa na wizara ya maji,kwa lengo la kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.
 Chombo cha kisasa cha kunawia mikono kilichotolewa na wizara ya maji kwa ajili ya shule ya sekondari Tumani tarafa ya Kinampanda wilaya ya Iramba.Picha zote na Nathaniel Limu.

No comments: